Sehemu ya Darasa la Vijana wa Shule za Msingi kutoka sehemu mbalimbali.
Meneja
Mradi wa Aitel & DTBI Computer Lab, Agape Jengela akizungumzia
kuhusu mradi huo wa Airtel Fursa ambao umenza na Darasa la
Vijana wa Shule za Msingi kutoka sehemu mbalimbali
za jiji la Dar es Salaam, katika fursa hiyo Watoto wamejifunza
kutengeneza ROBBOT.
Sehemu ya Darasa la Vijana wa Shule za Msingi kutoka sehemu mbalimbali.
Sehemu ya Darasa la Vijana wa Shule za Msingi kutoka sehemu mbalimbali.
Sehemu ya Darasa la Vijana wa Shule za Msingi kutoka sehemu mbalimbali.
Sehemu ya Darasa la Vijana wa Shule za Msingi kutoka sehemu mbalimbali.
Vijana Dar waanza Masomo ya Tehama
Kampuni yasimu za mkononi ya Airtel kwa kushirikiana na Atamizi ya Teknohama ya Dar es Salaam (DTBi)
imeanza
kutoa mafunzo ya Tehama kesho katika maabara ya kompyuta iliyopo katika
shule ya msingi kijitonyama na kuwawezesha vijana zaidi ya 20
waliojiandikisha kuanza
kupata mafunzo hayo.
Mafunzo
hayo yameanza kufatia Airtel na DTBi kutangaza kuanza kwa mafunzo hayo
na kuwaalika vijana kuanzia ngazi ya shule za msingi,sekondari, vyuo
vikuu na wafanya biashara kujiandikisha na kufaidika na mafunzo
haya yatakayowasaidia kuvumbua application mbalimbali, kuwapatia vijana
ujuzi katika mswala ya Tehama na pia kuwawezesha vijana wajasiriamali
kuendesha shughuli zao za kibiashara kwa kutumia technologia za kisasa
Akiongea
kuhusu kuanza kwa mafunzo hayo, Meneja Mradi wa Airtel Bi Jane Matinde
alisema, Tumefurahishwa sana na muitikio mkubwa uliofanya na vijana
hususani wa shule hii ya msingi ya kijitonyama na watoto
kutoka maeneo mengine katika kujiandikisha na kuanza mafunzo haya.
Tayari tunao jumla ya wanafunzi 20 ambapo wamejipanga kuanza kujifunza
kesho kuanzia saa 9 mchana hadi saa 11 jioni. Tunaamini hii ni fursa
muhimu sana kwa vijana wetu wenye kuonyesha dhamira
yao ya kubobea katika maswala ya Tehama na komputa ya sayansi kuanza
sasa wakiwa katika umri mdogo.
Bado
tunapokea maombi ya kujiunga hivyo tunatoa wito kwa vijana wa sekondari ,
wale waliomaliza darasa la saba , wafanyabiashara kutumia vyema maabara
hii yenye lengo la kuwezesha jamii hususani vijana kuongeza
ujuzi na ueledi kwenye maswala ya technologia na Tehama kwa ujumla.
Kwa
upande wake Meneja wa maabara ya Airtel Fursa , Agape Jengela alisema “
Tayari tumejipanga kutoa mafunzo kwa vijana, walimu wamejipanga vyema
katika kuhaikisha
vijana hawa wanapata mafunzo bora. Mafunzo hayo ni pamoja na
lego Robotics, program za uhuishaji kwa watoto(ziitwazo scratch) na
ubunifu na uchapishaji wa“3D objects” msingi wa kompyuta, uelewa wa
kompyuta, kutengeneza program mbali mbali
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.