Mkuu wa Wilaya ya Kibaha
Assumpter Mshama
akizungumza na waandishi wa habari Ofisini kwake kuhusina na kulaani
matukio ya vitendo vya kushambuliwa kwa viongozi kwa risasi, utakeji
wa watoto
sambamba na kukemea tabia ya baadhi ya watu wanaotoa maneno machafu kwa
Rais Dk
Joh Pombe Magufuli.
(PICHA NA VICTOR MASANGU)
NA VICTOR MASANGU,
GSENGO BLOG
KIBAHA PWANI
MKUU wa Wilaya ya Kibaha Assumpter Mshama amelaani vikali vitendo vya
matukio ya baadhi ya watu kuwavamia na kuwashambulia kwa risasi viongozi na pia
hakusita kukemea tabia ya utekaji wa watoto pamoja na wale ambao wamekuwa wakimtolea
maneno machafu Rais wa awamu ya Tano Dk John Pombe Magufuli kitu ambacho kinamuumiza
na anachukizwa nacho.
Akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake kuhusiana
na matukio yanayoendelea katika sehemu mbali mbali Mkuu huyo alisema kwamba
anasikitishwa kuona vitendo kama hivyo vinaendelea kufanyika katika jamii ya
watanzania hali ambayo inachangia kwa kiasi kikubwa kwa wananchi kuishi wakiwa katika hali ya hofu.
Mkuu huyo alisema kuwa baadhi ya watu kwa sasa wamekuwa wakiamua kumtolea maneno machafu
kiongozi wan chi bila ya kufahamu kuwa ni kinyume kabisa na sheria na taratibu
za nchi kwa hivyo tabia kama hiyo haifai hata kidogo katika jamii na badala
yake watanzania wanatakiwa kuwa wazalendo na nchi yao.
“Hivi karibuni ndugi waandishi mimi nachukizwa sana na kuona
matukio mbali mbali yaiendelea hapa nchini, kama vile watoto kutekwa nyara,
baadhi ya viongozi kupigwa risasi kwa kweli hii sio sahii kabisa hta kidogo na
wengine kutoa maneno machafu kwa kiongoiz wetu wa nchi kwa hili mimi nina laani vikali kabisa .
“Na kitu kingine napenda kuchukua fursa hii kumpa pole
Mwanasheria wa Chadema Tundu Lissu kwa kuvamiwa na kushambuliwa na risasi za
moto na kumjeruhi vibaya na watu wasiojulikan,
huyu Tundu Lissu ni kiongozi mkubwa na ni mtu maarufu zana hapa kwentu Tanzania
lakini kitendo cha kushambuliwa na risasi sio sahii hata kidogo na mimi
namwombe kwa Mungu apone na arudi kuendelea na Majukumu yake ya kuwatumbikia
wananchi wa jimbo lake,”alisema.
Pia katika hatua
nyingine amebainisha kuwa serikali Wilayani Kibaha Mkoani Pwani inatarajia kuvifutia rasmi hati viwanja zaidi ya 754
ambavyo baadhi ya watu wamevitelekeza na
kushindwa kabisa kuviendeeza kwa kipindi
cha muda mrefu hali ambayo imepelekea
kwa sasa maeneo mengine yamegeuka kuwa ni vichaka na mapori makubwa ambayo yamekuwa ni kimbilio la
kujifichia wahalifu pindi wanapofanya matukio ya wizi.
Tamko hilo limetolewa na Mkuu wa Wilaya ya Kibaha Assumpter
Mshama wakati alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake kuhusiana na changamoto mbali mbali zilizopo
katika suala la umiliki wa maeneo pamoja na mikakati waliyojiwekea katika
kuhakikikisha maeneo ambayo hayaendelezwi yanarudishwa katika mikono ya
serikali.
Mkuu huyo wa Wilaya alibainisha kwamba katika kuhakikisha
anakabiliana na tatizo hilo tayari
ameshamwandikia barua Waziri wa ardhi William Lukuvi kwa lengo la kuweza kumjulisha orodha ya watu
ambao wameshindwa kabisa kuviendeleza viwanja hivyo hadi kufikia hatua ya kuwa
mapori makubwa.
Nao baadhi ya wananchi Wilayani Kibaha Mkoa wa Pwani akiwemo
Elfasi Msuya na Zakharia Cheze wakizungumza na mwandishi wa habari hizo kuhusina
na tamko la Mkuu wa Wilaya kufuta umiliki wa viwanja visivyoendelezwa
wamepongeza hatua hiyo ya serikali kwani
itaweza kuwapa fursa wananchi wa hali ya chini waweze kujenga makazi ya kuishi.
WILAYA ya Kibaha mkoani Pwani kwa sasa
bado inakabiliwa na changamoto ya kuwa na idadi kubwa ya
viwanja ambavyo vimetelekezwa na kutoendelezwa kwa zaidi ya miaka 15
hivyo kusababisha kuwepo kwa vichaka na mapori makubwa ambayo
yanahatarisha usalama wa
wananchi kutokana na wahalifu kujificha katika maeneo hayo.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.