Rais Uhuru Kenyatta wa Kenya amesema kuwa, alihisi uchungu mwingi baada ya Mahkama ya Kilele nchini humo kufuta ushindi wake katika uchaguzi uliopita wa tarehe Nane Agosti mwaka huu.
Aidha Rais Kenyatta amesema kuwa, hana
chuki na jamii ya Wakisii ambayo anatokea Jaji Mkuu David Maraga
aliyefuta ushindi wake, ingawa amesisitiza kwamba, anapinga uamuzi wa
jaji huyo. "Hebu chukulia kama umenunua ng'ombe kisha akaibwa,
hatimaye polisi wakampata na walipompeleka mahakamani jaji akasema kwa
sababu fomu ya 'P3' haikujazwa hivyo ng'ombe huyo anatakiwa arejeshwe
kwa mwizi."
Akisisitiza kuwa hana chuki na jamii ya
Kisii Rais Uhuru Kenyatta amesema: "Sina shida kamwe na jamii ya Kisii
lakini nina shida na mahakama na huyo mzee kwa uamuzi wake. Nikikosa
kujitetea watu watadhani ni kweli niliiba. Lazima nijitetee, hata wewe
ukifanyiwa dhambi sharti ujitetee. Lakini pia hatutaki siasa za ukabila.
Hatutaki kurudi huko tena, tulipoteza uhai wa Wakenya na mali zetu.
Tukashifu siasa zinazoendeshwa kwa msingi wa ukabila," Alisema Rais
Kenyatta.
Awali
Muungano wa National Super Alliance (NASA) ulipinga ushindi wa Rais
Kenyatta aliyepeperusha bendera ya chama cha Jubilee katika uchaguzi wa
Agosti nane, ambapo hata hivyo Mahakama ya Kilele ya nchi hiyo ilikubali
malalamiko ya muungano huo wa upinzani na kufuta ushindi wake. Katika
malalamiko yake mahakamani NASA ilihoji fomu 34A na 34B kwamba
zilikuwa na dosari kwa kutotiwa sahihi na mawakala huku zingine zikikosa
kujazwa matokeo kando na kutokuwa na alama za usalama.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.