Wananchi na madiwani wakiwa wameweka Mawe kabla ya kutawanywa . |
Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Geita,Elisha Lupuga akiwa kwenye kikao wakati alipokuwa akielezea namna ambavyo wameweza kufukuzwa na jeshi hilo. |
Mkuu wa Wilaya ya Geita Mwl,Herman Kapufi akizungumza na kutoa maelekezo ya namna ya kufanya wakati wa kikao hicho. |
Baadhi ya wajumbe wa kikao hicho wakimsikiliza Mkuu wa Wilaya wakati alipokuwa akiwakilisha maamuzi ambayo wameyachukua. |
Mkuu wa Mkoa wa Geita Meja Jenerali Mstaafu Ezekiel Kyunga akiwasisitiza kutulia na kuachana na ghasia wasubilie meza ya mazungumzo na Naibu waziri wa Nishati na madini siku ya Jumatatu. |
Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoani Geita Mponjoli Mwabulambo akisisitiza kutokukubaliana na madiwani juu ya tukio ambalo wamefanya siku ya leo. |
Jeshi la Polisi Mkoani Geita limelazimika kutumia mabomu ya
machozi na kupiga risasi za moto hewani kwaajili ya kuwaondoa waandamanaji
ambao walikuwa wakiongozwa na madiwani wa halmashauri mbili ambazo ni ya mji na
Wilaya ya Geita ambao walikuwa wametanda kwenye barabara ya mgodi huo wakizuia
magari kuingia na kutoka Kampuni ya uchimbaji madini ya dhahabu ya Geita (GGM),wakishinikiza kulipwa
deni wanaloidai GGM kiasi cha zaidi ya Dola Bilioni 12.65
Tukio hilo limetokea
leo (jana) majira ya saa mbili na nusu asubuhi wakati madiwani hao na
wananchi wakiwa wamefunga barabara ya
mgodi wakishinikiza kulipwa deni hilo kufuatia maazimio ya kikao maalumu cha
baraza la madiwani kilichokeiti juzi.
Azma ya kukata mawasiliano ya barabara na vyanzo vya maji
zilianza saa 10.00 usiku ambapo madiwani waliweka mawe katika njia kuu za kuingia
mgodini humo na kwenye chanzo cha maji kilichopo Nungwe.
Baadi ya madiwani ambao wamzungumza na Maduka online Joseph
kwenye eneo la tukio baada ya kutawanywa na mabomu ya machozi Sasembe
Kaparatusi na Constantine Molandi ambaye ni makamu mwenyekiti wa
halmashuri ya mji wa Geita wamesema kuwa walikubaliana jana (juzi) kwenye vikao
vya chama ngazi ya wilaya na mkoa pamoja na baraza
maalum kuwa leo watafanya maandamano ya amani kwa lengo la kushinikiza kudai deni hilo huku wakilaani
kitendo cha jeshi hilo kutumia nguvu kubwa.
“Tulikubaliana kwenye vikao ngazi ya chama wilaya ,na mkoa na baraza maalum la
madiwani na uongozi wa wilaya
pamoja na mkoa unafahamu
kuwa leo tunaandamana kudai haki lakini cha kushngaza askari polisi wametutawanya kwa mabomu “ alisema Kaparatus .
Kabla ya kutawanywa waaandamanaji hao,Mbunge wa jimbo la
Geita Bw. Joseph Kasheku Msukuma ameiambia maduka online kuwa amesikitishwa na Kamanda Mkuu wa Polisi
kumtuhumu kuwa yeye ndiye mchochezi mkuu wa mgogoro huo.
“Nashangaa sana RPC anakuwa na chuki na mimi kwani kuwa
Mbunge ni tatizo kwani ubunge alinipa yeye hata kama nikiacha ubunge nina
maisha yangu na awezi kusema kuwa ccm ni kielele yani kweli sisi ni kielele”alisema
Msukuma.
Ameonezea kuwa kiasi cha fedha zinazodaiwa zinatakiwa kulipwa
kwani zimekuwa za muda mrefu na zinaweza kusaidia katika swala la maendeleo.
Hata
hivyo amemtaka Kamanda Mponjoli kuomba
radhi kwa Chama Cha Mapinduzi ccm na kwa
serikali kwa ujumla kutokana na kauli mbaya alizotoa, akiongeza kuwa
ameidhalilisha chama hicho.
“Kwa
kauli hiyo inadhihirisha wazi kuwa Polisi wanakuwa na upande wakati wanapoenda
eneno la kazi na hilo halitakiwi na kwa kutuuliza kwa dhihaka iwapo sisi ni CCM
ama siyi, hiyo kauli ni mbaya sana kwani sisi tulikuwa tukidai haki ya kodi
hiyo kwa niaba ya wananci wetu.
Mkuu
wa Mkoa wa Geita, Meja Jenerali mstaafu Ezekiel Kyunga, ambaye aliwalaumu
madiwani hao kwa kitendo cha kukata bomba la maji katika chanzo cha maji cha
Nungwe, aliingilia kati suala hilo akashauri kuwa ni vyema shauri hilo
likamalizwa kwa kutumia busara kwa manufaa ya wana Geita.
“Waheshimiwa
Madiwani tuweke mbele hekima na busara, tuweke mbele huduma za jamii, za mgodi wa GGM na wananchi kwa jumla
ziendelee kwa amani hebu tuwe watulivu wakakti tukitafuta suluhu, kudai haki ni
sawa lakini ni njia zipi mnatumia kuzidai, tuache kudai haki kwa njia ya fujo
ya aina hii kwani sheria za nchi haziruhusu,”alisema.
Kwa upande wake mkuu wa wilaya ya Geita Mwl..Herman Kapufi
amesema suala hilo limefikishwa katika wizara ya nishati na madini na kwamba
jumatatu ya wiki ijayo Naibu waziri akiambatana na Kamishina wa madini watafika
mkoani Geita kukutana na pande zote kwaajili ya kutafuta suluhu
“Hata hivyo
tumewasiliana na Naibu Waziri wa Nishati na Madini, Dk. Mendrad Kalemani juu ya suala hili ambapo
tumekubaliana kukutana jumatatu ijayo, akiambatana na Kamishna wa madini ambapo tutakaa nao pamoja na GGM ili kujadili suala hili”Alisema Kapufi.
Licha ya ahadi hiyo ya Viongozi kutoka kwenye wizara husika,
Mwenyekiti wa chama cha Mapinduzi CCM wilaya ya Geita Barnabas Mapande akaomba
kutoa taarifa kwa mkuu wa wilaya kuwa kamanda wa jeshi la Polis mkoani humo
anawatetea wawekezaji hasa GGM ambao wameshindwa kulipa fedha za kuharakisha
maendeleo ya Mkoa
Naye Mkuu wa mkoa huo Meja jenerali mstaafu Ezekiel
Kyunga,amesema njia pakee ya kumaliza mgogoro huo ni kufuata sheria,kanuni na
taratibu bila kuathiri shughuli za kijamii na huduma kwa wananchi na kwamba
njia iliyotumiwa na madiwani kudai haki yao si sahihi.
Akizungumza na waandishi wa habari Kamanda wa Jeshi la
Polisi Mkoa wa Geita,Mponjoli Mwabulambo amesema hayupo tayari kuomba radhi
kwani swala hilo na mkusanyiko huo umefanyika kinyume cha sheria na kwamba
hakuna lugha ambayo ametumia kukikashifu chama cha mapinduzi CCM.
IMEANDALIWA NA MADUKA ONLE.
IMEANDALIWA NA MADUKA ONLE.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.