Naibu Waziri wa Afya,Mendeleo ya jamii jinsia, wazee na Watoto, Dk. Hamisi Kigwangalla akikagua mfumo wa maji ndani ya chumba cha upasuaji Hospitali ya Mkoa wa Mara wakati alipotembelea Hospitali hiyo majira ya usiku jana
Naibu Waziri wa Afya,Mendeleo ya jamii jinsia, wazee na Watoto, Dk. Hamisi Kigwangalla akihoji uchafu uliokuwa ndani ya chumba cha upasuaji Hospitali ya Mkoa wa Mara wakati alipotembelea Hospitali hiyo majira ya usiku jana
Baadhi ya vitu vilivyokuwa ndani ya chumba cha upasuaji cha hospitali ya Mkoa wa Mara, hali hiyo ni kinyume na utaratibu wa vyumba vya upasuaji
Naibu Waziri wa Afya,Mendeleo ya jamii jinsia, wazee na Watoto, Dk. Hamisi Kigwangalla akikagua maeneo chumba hicho cha upasuaji huku akipata maelezo.
Naibu Waziri wa Afya, Mendeleo ya jamii jinsia, wazee na Watoto, Dk. Hamisi Kigwangalla akitoa maelekezo kwa Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Mkoa wa Mara
Naibu
Waziri wa Afya,Mendeleo ya jamii jinsia, wazee na Watoto, Dk. Hamisi
Kigwangalla amekerwa na uchafu ulioko katika vyumba vya upasuaji vya
hospitali ya rufaa ya Musoma na zahanati ya Murangi na vyumba hivyo
kubadilishwa stoo na eneo la taka.
Naibu
Waziri ambaye Mkoani Mara kwa ziara ya kikazi ya siku nne alifanya
ziara ya kushtukiza katika hopsitali ya rufaa ya Musoma na kubaini
uchafu uliopo katika chumba cha upasuaji kilichozinduliwa mwaka jana kwa
mashuka na mipira yake kuwekwa chini na huku kukiwa na vifaa vya
kuwekea mashuka hayo.
‘’Hivi
ndivyo mnatunza vitu vya upasuaji kweli,matroni hivi,kuna sababu gani
ya nyie kuondoka hapa,mali ya umma inaharibiwa hivi, hamna uchungu
jamani, sisi sote ni watanzania, leo mimi naweza kuugua hapa, Mkuu wa
Mkoa au mwanachi,kwa hali hii hapa kun ahuduma kweli..na hii eti ndo
hopspitali ya rufaa ambayo mtu akizidiwa huku pembeni analetwa hapa?
Alihoji Kigwangalla na kuonyesha masikitiko makubwa.
Aidha
aliagiza Katibu Tawala wa Mkoa, Adoh Mapunda kuajiri Mganga mfawidhi wa
hospitali (Medical officer Incharge) mpya atakayesimamia hospitali
hiyo.
Sanjali
ya hayo alishangazwa pia kuona chumba hicho mabomba na masinki yakiwa
mabovu na ukosefu wa taa katika chumba cha kutokosea vifaa,
(stearlization Room) vifaa vya kubebea madawa ambavyo vinanesa nesa na
vifaa vya kuchemshia vifaa vya upasuaji vikiwa chakavu na sehemu ya
kuwekea vifaa hivyo ikiwa pia chakavu.
Akiwa
katika chumba cha upasuaji cha Murangi alipokelewa na harufu za damu
iliyooza na harufu ya popo,huku vifaa vya kutupia taka zikiwa ni ndoo za
mafuta ya kupikia na kuagiza pia usafi ufanyike na kuondolewa kwa
kinyesi cha popo na kuziba maeneo wanayopita kwani sehemu hiyo
inatakiwa kuwa na usafi wa hali ya juu.
Aidha
aliagiza kuwepo kwa mtaalamu wa mashine mpya iliyopo katika chumba
hicho,na mashine ya usingizi,(Anaesthesia Machine), kwani hakuna
mtaalamu na kuwekwa mfumo wa computer ili kukusanya mapato halisi.
Akiwa katika wodi ya wazazi aliwasalimu wazazi waliojifungua siku hiyo na kuwaombea afya njema.
Nao
Wazazi, Nyachiro Phares wa kata ya chumwi aliyejifungua siku hiyo mtoto
wa kike na Sikujua Goda wa Kata ya Musanja aliyejifungua mtoto wa kiume
waliipongeza Serikali kwa jitihada zake za kuhakikisha Mwanamke
anajifungua salama kuliko hapo awali ambapo walikuwa wanajifungua
nyumbani hali ambayo ilikuwa inahatarisha afya na usalama wao.
Akizungumza
mara baada ya Naibu Waziri kutembelea wodi ya wazazi,chumba cha
upasuaji na Maabara, Mjumbe Mkutano Mkuu UWT Taifa kutoka Wilaya ya
Musoma, Eva-Sweet Musiba alimpongeza Naibu waziri huyo kwa ziara yake
Mkoani Mara ambayo italeta chachu ya kufanya kazi kwa uadilifu na si
kwa mazoea ambayo yalikuwa yamekidhiri.
Aidha amewataka akina Mama kuipenda Serikali ya awamu ya Tano kwani inajali akina mama, wazee na watoto.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.