Mtoto mchanga wa kike anayekadiliwa kuwa na umri wa siku moja ameokotwa kwenye shimo la choo kinachotumika katika mtaa wa Lumala Kata ya Kawekamo Wilayani Ilemela mkoani Mwanza akiwa hai baada ya kutupwa na mzazi wake.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza, Ahmed Msangi amethibitisha
kutokea kwa tukio hilo na kusema baada ya muda mchache kupita toka
kichanga hicho kutupwa kwenye shimo hilo la choo, polisi walipata
taarifa na kwenda kusaidia kumtoa mtoto huyo ambaye sasa amepelekwa
hospitali ya Sekou Toure kwa matibabu zaidi.
“Inadaiwa kuwa baada ya muda mchache kupita toka mtoto alipotupwa,
palikuwa na mtu aliyekwenda kujisaidia chooni ndipo akiwa chooni
alisikia sauti ya mtoto mchanga akilia toka ndani ya shimo la choo.
Inasemekana kuwa baada ya mtu huyo kusikia sauti hiyo ya mtoto akilia,
alikwenda kutoa taarifa kwenye uongozi wa serikali za mtaa ambapo
uongozi wa mtaa ulifika mahali hapo kisha ulitoa taarifa kituo cha
polisi” alisema Msangi na kuongeza;
“Askari baada ya kupokea taarifa hiyo walifanya ufuatiliaji wa
haraka hadi eneo la tukio na kushirikiana na wananchi waliokuwepo eneo
hilo na kufanikiwa kutoa kichanga hicho cha mtoto toka ndani ya shimo la
choo kikiwa hai. mtoto amepelewa hospitali ya mkoa ya sekou toure
kupatiwa matibabu na hali yake inaendelea vizuri.
Polisi wapo katika
upelelezi na msako katika maeneo mbalimbali ya mkoa wa Mwanza, ili
kuweza kubaini mzazi/wazazi wa mtoto huyo ambao wamefanya ukatili huo
dhidi ya mtoto, ili baadae waweze kufikishwa kwenye vyombo vya sheria
ili hatua stahiki za kisheria ziweze kuchukuliwa dhidi yao na iwe
fundisho kwa wengine”.
Kamanda Msangi ametoa wito kwa wazazi na walezi kuacha tabia ya
kutenda ukatili dhidi ya watoto ikiwepo vitendo vya kutupa watoto kwani
ni kosa la jinai na endapo mtu atabainika kufanya hivyo hatua kali za
kisheria zitachukuliwa dhidi yake.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.