TAREHE
24.09.2017 MAJIRA YA SAA 08:00HRS ASUBUHI KATIKA KIJIJI CHA MWAGILIGILI KATA YA
NHUNDULU WILAYA YA MISUNGWI MKAO WA MWANZA, KWILOKEJA BONIPHACE, MIAKA 35,
MKAZI WA KIJIJI CHA MWILIGILIGILI, ANATUHUMIWA KUMUUA MKEWE AITWAE SHIJA
LUCHAGULA, MIAKA 30, MKAZI WA KIJIJI CHA MWAGILIGILI, HII NI BAADA YA KUZUKA KWA
UGOMVI KATI YAO ULIOTOKANA NA WIVU WA KIMAPENZI KISHA KUMPIGA FIMBO SEHEMU
MBALIMBALI YA MWILI WAKE KISHA KUMNYONGA HADI KUFA NA BAADAE YEYE MWENYE KWENDA
KUJINYONGA HADI KUFA, KITENDO AMBACHO NI KOSA KISHERIA.
INASEMEKANA KUWA
MTUHUMIWA WA MAUAJI HAYO ALIKUWA AKIMTUHUMU MKEWE KUWA ANATOKA NJE YA NDOA HALI
ILIYOPELEKEA KUZUKA KWA UGOMVI WA MARA KWA MARA BAINA YAO. INADAIWA KUWA KABLA
YA TUKIO HILO LA MAUAJI KUTOKEA SIKU HIYO MTUHUMIWA ALIAMKA ASUBUHI NA KUFAGIA
UWANJA WA NYUMBA YAO KAMA MTEGO WA KUBAINI WATU WANAOKUJA HAPO NYUMBANI KWAKE, KISHA
ALIKWENDA KWENYE SHUGHULI ZAKE ZA KAWAIDA.
INADAIWA KUWA BAADA YA MUDA MCHACHE KUPITA MTUHUMIWA
ALIRUDI NYUMBANI, NDIPO AKIWA HAPO NYUMBANI KWAKE ALIONA MATAIRI YA BAISKELI
KATIKA UWANJA WA NYUMBA YAKE NDIPO ULIZUKA UGOMVI KATI YAKE NA MKEWE HUKU AKIMTUHUMU
MKEWE KUWA ALIKUWA SI MWAMINIFU KATIKA NDOA HAPO NYUMBA KWAKE NA KUPELEKEA
KUMPIGA MKEWE HADI KUMUUA NA YEYE MWENYEWE KUJINYONGA HADI KUFA.
POLISI WANAENDELEA NA
UCHUNGUZI KUHUSIANA NA VIFO HIVYO, MIILI YA MAREHEMU TAYARI IMEFANYIWA
UCHUNGUZI NA KUKABIDHIWA KWA NDUGU WA MAREHEMU KWA AJILI YA MAZISHI.
KAMANDA WA POLISI
MKOA WA MWANZA NAIBU KAMISHINA WA POLISI ANATOA WITO KWA WAKAZI WA JIJI NA MKOA
WA MWANZA, HUSUSANI WANANDOA AKIWATAKA KUACHA TABIA YA KUJICHUKULIA SHERIA
MKONONI PINDI WANAPOKUWA KWENYE MIGOGORO YA NDOA, BALI WAWAHUSISHE WAZEE WENYE
HIKIMA NA BUSARA PAMOJA NA VIONGOZI WA DINI NA
SERIKALI ILI KUEPUSHA MAJERUHI NA
VIFO VYA AINA KAMA HII VINAVYOWEZA KUEPUKIKA.
IMETOLEWA NA:
DCP: AHMED MSANGI
KAMANDA WA POLISI (M)
MWANZA
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.