WAZIRI wa Elimu Profesa, Joyce Ndalichako (Kushoto)akiwa na Naibu Spika wa Bunge la Jamuhuri ya muungano wa Tanzania , Dkt.Tulia Akson , wakimkabidhi vitabu vya sayansi kwa Mkuu wa
sekondari ya Kayuki, Bertha Sarufu, vitabu vilivyotolewa msaada na kampuni ya
simu za mkononi ya Airtel. Mbali ya Kayuki, shule nyingine za sekondari
zilizonufaika na msaada huo ni Ikuti, Bujela, Ntaba na Ikapu, zote zipo
wilayani Rungwe. Airtel imekabidhi vitabu vya sayansi mwishoni mwa wiki vyenye
thamani ya shilingi milioni 15.
WAZIRI wa Elimu Profesa Joyce Ndalichako pamja na Naibu Spika wa Bunge, Dkt.Tulia
Akson wakipokea vitabu vya masomo ya sayansi vilivyotolewa msaada na kampuni ya simu za
mkononi ya Airtel.Anayewakabidhi vitabu hivyo ni Meneja
mauzo wa Airtel mkoa wa Mbeya bw, Bartholomew Masatu. Airtel imekabidhi vitabu
hivyo mwishoni mwa wiki hii ikiwa ni ahadi yake ya kuendeleza masomo ya sayansi
nchini.
Press Release
Airtel yatoa vitabu masomo ya sayansi vya thamani ya shilingi
milioni 15 kwa shule za sekondari Mbeya
- Shule tano kufaidika na vitabu vya sayansi vyenye thamani ya shilingi milioni 5
Mbeya; Katika
kuinua sekta ya elimu nchini , kampuni ya simu za mkononi ya Airtel leo imetoa
msaada wa vitabu vya sayansi vyenye thamani ya shilingi milioni 15 kwa shule 5
za sekondari mkoani Mbeya
Vitabu hivyo vimetolewa na Airtel kwa kushirikiana na
Tulia Ackson foundation kwaajili ya shule za sekondari za Ikuti,
Kayuki , Bujeli, Ntaba na Ikupa
Akiongea wakati wa hafla ya kukabidhi vitabu, Naibu
Spika Mh Dkt, Tulia Ackson alisema aliwapongeza Airtel kwa kushirikiana na
taasisi yake ya Tulia Ackson ili kusaidia shule za sekondari zenye uhaba wa
nyenzo za kujifunzia mkoani Mbeya. Dr. Ackson alisema” ni muhimu kwa makapuni
binafsi ya umma kushirikiana katika kuinua sekta ya elimu nchini
ili kuweka mazingira bora kwa wanafunzi kujifunza na hivyo kuongeza uelewa na
kuwa na taifa lenye ueledi
Tumeshuhudia uhaba mkubwa wa vitabu katika mashule
ambapo uwiano upo kati ya kitabu kimoja kwa wanafunzi 5 hadi 10.
Tunaamini msaada huu tunaoutoa leo utasaidia kuzalisha nguvukazi yenye ueledi
itakayowawezesha kujiajiri au kuajiriwa na kujenga uchumi wenye nguvu. Natoa
wito kwa makapuni mbalimbali kuungana nasi na kuzifikia shule zenye
uhitaji wa vifaa vya kufundishia nchini
Kwa upande wake Meneja Mauzo mkoani Mbeya, Bartholomew
Masatu alisema” Airtel tunaamini jamaa iliyoelimika inajengwa kutoka katika
shule zenye vifaa vya kufundishia vyakutosha hususani vitabu. Ili kuwa na
maendeleo endelevu ni muhimu kuwekeza kwenye elimu na leo tunathibitisha
dhamira yetu kwa kutoa msaada wa vitabu katika shule hizi hapa Mbeya”.
Tunaamini msaada utachochea ufaulu mzuri katika masomo
ya sayansi katika mkoa wetu.” Aliongeza Masatu
Kwa upande wake Mwalimu Mkuu wa sekondari ya
Kayuki Bi Bertha Sarufu Kwa niaba ya shule zilizofaidika na
msaada wa vitabu alisema “ Tunashukuru sana Airtel kwa kutufikishia msaada huu na
napenda kutoa wito kwa wanafunzi kuvitunza na kuvitumia vitabu hivi kwa lengo
la kuboresha ufaulu. Msaada huu umekuja wakati muafaka wakati shule zetu
zimekuwa na upungufu wa vitabu na tunaahidi kuvitunza na kuvitumia
ipasavyo".
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.