Makamu
wa Rais apongeza kampeni dhidi unyanyapaa kwa wanawake wenye tatizo la ugumba.
·Kampeni hiyo ni hatua
sahihi katika kupunguza unyanyapaa unaohusiana na ugumba
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu
Hassan amezipongeza juhudi zinazofanywa na taasisi ya Merck ambayo
ni kampuni inayoongoza katika sayansi na teknolojia ambayo
imelenga kushughulikia masuala uwezeshwaji wa wanawake na
huduma za afya akisema kwamba wamekuja nchini kwa wakati mwafaka
Wakati
wa mkutano maalum kati ya Makamu wa Rais Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan na
Ofisa Mtendaji Mkuu wa Merck Foundation Makamu wa
Rais alisema kuwa Merck Foundation inakaribishwa na
serikali inatarajia kushirikiana na taasisi hiyo inayoheshimika
na iliyo makani katika kuwezesha wanwake , vijana, huduma za
afya na sayansi.
Tunatambua
mchango unaotolewa na Merck Foundation katika kujengea
uwezo huduma za afya barani Afrika na tunakaribisha shughuli
zake nchini Tanzania, hususani katika kampeni
zinazolenga kuuongezea umma uelewa kuhusu ugumba.
Makamu
wa Rais aliongeza, “Mimi binafsi nitafanya kazi na Merck katika
kuwawezesha wanawake walio na uwezo duni kijamii na kiuchumi kote nchini
Tanzania na sehemu nyingine duniani ili kujenga utamaduni
mpya katika kuheshimu na kumtambua wanawake kama sehemu
ya wanajamii wanaozalisha wawe ni kinamama na hata wasio wazazi.”
Merck
Foundation hali kadhalika imejikita katika ushirikiano wa muda mrefu
na serikali ya Tanzania katika kuijengea uwezo katika huduma za
afya na kuboresha kufikiwa kwa ubunifu na
masusluhisho yaliyo katika uwiano kote nchini ikiwa ni
sehemu ya program za uwajibikaji kwa jamii barani Afrika.
“Merck
Foundation itatilia mkazo katika uwezeshwaji wa wanawake walio na tatizo la
ugumba kupitia upatikanaji wa taarifa, uelewa, afya, kubadili
mitazamo na kuwewawezesha kiuchumi kote nchini kupitia kampeni ya
Merck ya Zaiidi ya mama,” alisema Ofisa Mtendaji Mkuu wa Merck, Dk. Rasha
Kelej.
Kampeni
hiyo ambayo inatoa msukumu kwa vyombo vya habari na wadau
wengine kuchpisha na kuwasilisha mada kwa njia ya mtandao, video na
vipindi vya redio kuhusu masuala yanayohusu ugumba ilizinduliwa nchini
Tanzania Juni mwaka huu. Washindi katika kampeni hiyo wanatarajiwa
kuondoka na zawadi ya fedha kuanzia dola 1000 hadi dola
5000.
“Tatizo
la ugumba barani Afrika ni kubwa, inakadiriwa kuwa mtu mmoja kati ya
kila watu wane walio na umri wa kuzaa anasumbuliwa na tatizo
la ugumba, na takribani asilimia 85 wale walio na tatizo
la ugumba linatokana na ukosefu wa tiba kwa ugonjwa ambao unaweza
kutibika, hivyo kuongeza uelewa kuhusu kuzuia hali
hiyo kupiti vyombo vya habari vya ndani na mitandao ya jamii ni
hatua muhimu.”, alisema Dk. Rasha Kelej’’
Aliongeza,
“Kujenga uelewa kuhusu ugumba kwa wanaume kwani
ugumba una athari sawa kwa wanaume na wanawake, lakini wamekuwa
ndio wanaolaumiwa peke yao, wanatengwa na kudhalilishwa
ndani ya jamii zao. Kampeni itashughulikia mada hizi na kutoa msukumo kwa
wanaume kujadili kwa uwazi tatizo lao la
ugumba na kushirikiana katika safari ya kutambua ugumba
na matibabu ya wake zao.”
Kwa
upande mwingine Merck foundation itajikita zaidi katika kugharamia mafunzo kwa
wataalamu wa afya kwenye maeneo ya saratani kwa watoto (paediatric oncology)
katika programu za udhamini nchini India, Ulaya na katika Chuo Kikuu cha
Nairobi kwa madaktari wa Tanzania ili kuboresha upatikanaji wa huduma zote
zinahusu saratani.
Hivi
karibuni Merck ilizindua Tuzo ya Kuvitambua Vyombo vya Habari kupitia kampeni
yake ya “Zaidi ya Mama” ili kuwatuza waandishi wa habari na
wanafunzi wanaosomea uandishi wa habari katika eneo la Afrika Mashariki ambao
watakuwa wamefanya vizuri katika kuandika habari
zinazoelewesha, kuelimisha na kuhabarisha ambazo zitaweza
kujenga jukwaa la majadiliano kuhusu ugumba ndani ya Afrika. Hafla
ya kutoa tuzo hizo inatarajiwa kufanyika Oktoba mwaka huu 2017.
Lengo la
tuzo hizo ni kujenga uelewa kuhusu mchango muhimu ambavyo vyombo vya
habari vinaweza kuutoa katika kuondo unyanyapaa
uliojikita katika tatizo la ugumba. Hali
kadhalika zinalenga utamaduni mbovu wa kuwabagua na
kuwadhalilisha wanawake na papo hapo kuuelimisha umma kuhusu kuzuia
ugumba, kuisimamia hali hiyo na ugumba kwa wanaume. Nyongeza katika
kampeni hiyo ni kwamba inalenga kutoa msukumo kwa
wanawaume kujadili hali yao ya ugumba kwa uwazi, kuwasaidia wake zao
katika safari zao za kupimwa na kutibiwa.
Kufahamu
zaidi kuhusu program za Merck Foundation na mafunzo yao pamoja na fursa za
udhamini. Tafadhali tembelea tovuti yao www.merck-foundation.com na www.merckmorethanamother.com
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.