Serikali ya Korea Kaskazini imeionya Marekani isitumie njia za vikwazo zaidi wala za kijeshi dhidi ya Pyongyang.
Wizara ya Mambo ya Nje ya Korea
Kaskazini imetoa taarifa kuionya Washington kwamba, iwapo itatumia
vikwazo zaidi dhidi yake au njia ya kijeshi, basi itakabiliwa na jibu
kali zaidi. Taarifa iliyotolewa na wizara hiyo imesema kuwa, majaribio
ya kombora la balestiki yaliyofanywa hivi karibuni na Pyongyang ni onyo
kwa Marekani.
Ijumaa iliyopita, Korea Kaskazini
ililifanyia majaribio kombora lake la balestiki la kuvuka mabara kwenda
katika maji ya Japan. Baada ya jaribio hilo, Kim Jong-un, kiongozi wa
nchi hiyo alitangaza kuwa jaribio hilo limethibitisha kwamba, sasa ardhi
yote ya Marekani inaweza kulengwa kwa makombora ya Pyongyang.
Kwa mara kadhaa Korea Kaskazini imekuwa
ikisisitiza azma yake ya kuendelea kujiimarisha kijeshi kwa silaha za
nyuklia hadi pale Marekani na washirika wake watakapositisha vitisho
dhidi yake. Kombora la kuvuka mabara la Korea Kaskazini. |
Wakati huo huo, habari zinaarifu kwamba
raia wa Korea Kaskazini wamepatwa na ghururi hasa baada ya serikali ya
nchi hiyo kufanya jaribio la kombora jipya siku ya Ijumaa iliyopita.
Televisheni ya APTN imetangaza kuwa, baada ya jaribio hilo wakazi wa
miji kadhaa walikusanyika katika viwanja mbalimbali na kushangilia hatua
hiyo ambayo wameitaja kuwa ni ushindi mkubwa dhidi ya Marekani.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.