Afisa wa ngazi ya juu wa uchaguzi wa Kenya
leo amekutwa ameuawa siku tatu baada ya kutoweka. Hayo yameeleawa na
maafisa uchaguzi wa Kenya.
Kuuliwa kwa afisa huyo kumezidisha wasiwasi na hofu juu ya uwezekano wa kutokea machafuko kabla ya uchaguzi mkuu wa wiki ijayo.
Chris Msando aliyekuwa Mkuu wa Kitengo cha Habari, Mawasiliano na Teknoloijia katika Tume Huru ya Uchaguzi na Mipaka ya Kenya (IEBC) aliteswa kabla ya kuuawa. Hayo yameelezwa na kitengo hicho cha IEBC.
Wakenya ambao walikumbwa na ghasia nchini mwao baada ya uchaguzi mkuu
wa mwaka 2007, Jumanne wiki ijayo wataelekea katika masanduku ya
kupigia kura kumchagua Rais mpya, wabunge na magavana.Chris Msando aliyekuwa Mkuu wa Kitengo cha Habari, Mawasiliano na Teknoloijia katika Tume Huru ya Uchaguzi na Mipaka ya Kenya (IEBC) aliteswa kabla ya kuuawa. Hayo yameelezwa na kitengo hicho cha IEBC.
Mwenyekiti
wa Tume Huru ya Uchaguzi na Mipaka ya Kenya, Wafula Chebukat amesema
kuwa hakuna shaka kwamba afisa huyo aliteswa na kisha kuuliwa. Amesema
swali linaloulizwa sasa ni kwamba nani aliyemuuwa afisa huyo na kwanini?
Chebukati
ameiomba serikali kutoa ulinzi kwa wajumbe wote wa tume hiyo ili
kuhakikisha kuwa Wakenya wanakuwa na uchaguzi huru na wa haki.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.