CAPTIONS
IMG_0400
Viongozi
waandamizi kutoka TADB, Bw. Augustino Chacha (kushoto) na Bw. Albert
Ngusaru (wapili kushoto) wakizungumza na Wakufunzi kutoka NABARD, Dkt.
R.S. Reddy
(kulia) na Bw. M.R. Gopal (wapili kulia) wakati wa ufungaji wa
mafunzo ya awamu ya pili yanayohusiana na Kanuni za Ukopeshaji katika
Kilimo yaliyokuwa yanafanyika katika Hoteli ya Beachcomber Dar es
Salaam.
IMG_0401
Mkurugenzi
wa Mikopo na Biashara wa TADB, Bw. Augustino Matutu Chacha akizungumza
na washiriki wa mafunzo ya awamu ya pili yanayohusiana na Kanuni za
Ukopeshaji
katika Kilimo wakati wa ufungaji wa mafunzo hayo.
IMG_0402
Mshauri wa Kiufundi wa MIVARF, Bw. Ravi Malik akizungumza wakati wa ufungaji wa mafunzo hayo.
IMG_0403
Mmoja
wa washiriki wa mafunzo hayo, Bi. Vivian Sakoe kutoka Benki ya NMB
akizungumzia faida aliyoipata baada ya kuhudhuria mafunzo hayo.
IMG_0404
Mwakilishi
wa Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania
(TADB), Bw. Albert Ngusaru (watatu kushoto) akifunga rasmi mafunzo ya
awamu
ya pili yanayohusiana na Kanuni za Ukopeshaji katika Kilimo yaliyokuwa
yanafanyika katika Hoteli ya Beachcomber Dar es Salaam. Wengine pichani
ni wakufunzi na maafisa kutoka TADB na MIVARF.
IMG_0405
Mshiriki
kutoka TADB, Bibi Rosemary Gordon akipongezwa na Mkufunzi wa mafunzo
hayo, Dkt. R.S. Reddy mara baada ya kukabidhiwa cheti cha kufuzu Mafunzo
ya Awali
ya Kanuni za Ukopeshaji katika Kilimo.
IMG_0406
Mwakilishi
wa Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania
(TADB), Bw. Albert Ngusaru (kulia) akiwakabidhi zawadi ya shukrani
Wakufunzi
kutoka NABARD, Dkt. R.S. Reddy (kushoto) na Bw. M.R. Gopal (wapili
kushoto) baada ya kufunga rasmi mafunzo ya awamu ya pili yanayohusiana
na Kanuni za Ukopeshaji katika Kilimo.
TADB: “TENDEENI HAKI MAFUNZO YA UKOPESHAJI KATIKA KILIMO”
Na mwandishi wetu,
Benki
ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania (TADB) imewataka wahitimu wa mafunzo ya
Kanuni za Ukopeshaji katika Kilimo kuyatendea haki mafunzo hayo kwa
kutumia utaalamu
walioupata katika kuwahudumia wakulima wanaomba mikopo kwenye taasisi
zao.
Akizungumza
na wahitimu hao wakati wa ufungaji wa awamu ya pili ya mafunzo hayo,
Mwakilishi wa Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa TADB, Bw. Albert Ngusaru
amesema
kuwa wahitimu hao wanapaswa kutumia weledi katika utendaji kazi wao ili
waweze kuyatendea haki mafunzo hayo.
Bw.
Ngusaru ameongeza kuwa mafunzo hayo yaliyokuwa na lengo la kuwajengea
uwezo watoa huduma hasa kutoka mabenki na taasisi za kifedha nchini
kuweza kutoa
huduma kwa wakulima kwa wakati na kuzingatia tija wakulima nchini ili
kuunga mkono juhudi za Serikali katika kuchagiza na kusaidia Mapinduzi
ya Kilimo kutoka kilimo cha kujikimu kwenda cha kibiashara ili kuchangia
kwenye ukuaji wa uchumi na kupunguza umaskini.
“Nawaomba
mukayafanyie kazi kwa vitendo mafunzo haya ili kuchagiza malengo ya
Serikali katika kuchagiza na kusaidia Mapinduzi ya Kilimo kutoka kilimo
cha kujikimu
kwenda cha kibiashara ili kuchangia kwenye ukuaji wa uchumi na
kupunguza umaskini nchini,” alisema Bw. Ngusaru.
Kwa
upande wake Mkurugenzi wa Mikopo na Biashara wa TADB, Bw. Augustino
Matutu Chacha amesema kuwa TADB ipo tayari kushirikiana na Mabenki na
Taasisi za fedha
nchini katika kuwakopesha wakulima nchini ili kuharakisha
mapinduzi na maendeleo katika Sekta ya Kilimo, ambayo inaajiri
zaidi ya asilimia 75 ya watu wenye uwezo wa kufanya kazi nchini na pia
kutoa kiasi cha zaidi ya
asilimia 65 cha mali ghafi kwa ajili ya viwanda.
“Tupo
tayari kushirikiana na mabenki yote nchini katika kukopesha mnyonyororo
mzima wa sekta ya kilimo na mifugo hili kuunga mkono juhudi
za Serikali za kuinua ukuaji wa uchumi na kupunguza umaskini nchini,” alisema.
Akizungumzia
faida aliyoipata baada ya kuhudhuria mafunzo hayo, mmoja wa wahitimu
hao, Bi. Vivian Sakoe kutoka Benki ya NMB amesema kuwa mafunzo hayo
yamewajenga
katika kutoa huduma bora kwa wakulima ambao ndio walengwa wakuu wa
mikopo ya kilimo nchini.
“Tumepata
utaalamu wa hali ya juu sana kwa kujifunza na kufahamu kwa undani
vigezo vya kuzingatia wakati wa utoaji wa mikopo kwa wakulima ambavyo
hapo awali
hatukuwa nao, hakika tunaishukuru TADB kwa mafunzo haya,” alisema.
Mafunzo
haya yaliendeshwa kwa ushirikiano wa pamoja kati ya TADB, Benki ya
Taifa ya Kilimo na Maendeleo Vijijini India (NABAD) na Programu ya
Miundombinu ya
Masoko, Uongezaji Thamani Mazao na Huduma za Kifedha Vijijini (MIVARF)
na kuhudhuriwa na zaidi ya washiriki 50 kutoka taasisi
zinazojishughulisha na utoaji wa mikopo kwa wakulima nchini.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.