Na James Timber, Mwanza
Shirika la wasaidizi kisheria Jamii Bugogwa (WAJABU) Kata ya Bugogwa katika Wilaya ya Ilemela jijini Mwanza, wamewasilisha changamoto wanazokutana nazo wafanyakazi wa majumbani na sheria zinazopaswa kufuatwa
kwa waajiri na waajiriwa kwenye kikao cha Madiwani, Watendaji wa Kata na Afisa
Maendeleo Kata kilichofanyika katika ukumbi wa malezi na makuzi Bugogwa.
Mwenyekiti wa Kikao hicho Swila Dede ambaye ni Diwani wa Kata ya Shibula wilayani
Ilemela alisema kuwa sheria ya kumlinda mfanyakazi wa nyumbani ilitengenezwa mwaka 2011 na kusainiwa mwaka
2012 na imeleta matokeo chanya kwa
baadhi ya maeneo kutokana uhamasishaji wa hali ya juu, baada ya jamii kutoa
ushirikiano mkubwa.
Dede alisema kuwa changamoto zinatokana na Afisa watendaji
wa mitaa kubadilishwa yale maeneo na wenyeviti wa mitaa kuwa wapya na
kutokupata elimu iliyotolewa shirika hilo waliposaini sheria hiyo hapo awali.
“Baada ya Kusainiwa kwa sheria ya wafanyakazi majumbani
katika Jamii ya Bugogwa shirika lilihakikisha linatoa elimu huku wenyeviti wa
Mtaa na watendaji kata waliokuepo
wakitoa ushirikiano wa kutosha
ambao kwa sasa uongozi umebadilika baadhi ya maeneo na wengi wao kutokujua
elimu hiyo”, alisema Dede.
Afisa Mtendaji wa Kata ya Sangabuye Juma Ngoroma alisema baadhi wafanyakazi wa nyumbani
wanafanyiwa ukatili na waajiri wao na kutosema
kwa kuhofia kuachishwa kazi na kuwataka wafanyakazi hao watumie
kaulimbiu ya shirika hilo isemayo “vunja ukimya upate haki yako”.
Kwa upande wake Afisa Maendeleo Kata ya Shibula Benjamin
Prosper alilalamikia wanajamii ambao hawatoi ushirikiano kwa uongozi ili kuwabaini waajiri ambao
wanawanyanyasa watumishi wa majumbani.
“Kuna baadhi ya wananchi wamekuwa hawatoi ushirikiano kwa
uongozi ili kuwabaini waajiri wanaowanyanyasa wasaidizi wa nyumbani”, alisema
Prosper.
Hata hivyo Afisa Mtendaji wa Kata ya Bugogwa Rashid Sukwa
alitoa pendekezo la kuanzisha daftari la
kuwaorodhesha waajiri wanaofanya
vitendo vya ukatili dhidi ya waajiriwa ili jamii iwe wazi na kuwatambua
wanaofanya vitendo hivyo.
Mratibu wa Shirika la wasaidizi kisheria Jamii Bugogwa
(WAJABU) Kata ya Bugogwa katika Wilaya
ya Ilemela jijini Mwanza Emmanuel Mhoja, akiwasillisha changamoto za
watumishi wa kazi majumbani alisema baadhi ya watumishi wanalazimishwa kufanya
ngono na waajiri na pengine watoto wa waajiri.
Mhoja alisema kuwa watumishi wa majumbani wengi wao
hawana mishahara, kutokana na kutofunga
mikataba pale wanapopata ajira hizo na kuchangia kuwepo kwa ajira ya muda mfupi
na mimba katika umri mdogo.
“Wafanyakazi majumbani
wengi wao wanapata ajira bila ya mkataba jambo linalochangia kuwepo kwa
ajira kwa muda mfupi na bila ya malipo yoyote na kuchangia kuongezeka kwa
vijana wasio kuwa na ajira ya mazingira rafiki na salama”, alisema Mhoja.
Akitaja baadhi sheria ndogo ndogo ambazo zilitungwa kwa ajili ya kuwalinda watumishi wa
majumbani na jamii ya Bugogwa kusaidiwa na WAJABU ni mwajamii haruhusiwi
kuajiri mfanyakazi chini ya miaka 18, mkataba kati ya mwajiri na mwajiriwa ushuudiwe
na Mwenyekiti wa Mtaa, Mwajiri amtambulishe
mwajiriwa baada ya siku 3 kupewa
ajira kwa uongozi wa Mtaa na kata.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.