¨ MTU MMOJA AMEFARIKI DUNIA NA
WENGINE WAWILI KUJERUHIWA KATIKA AJALI YA MOTO ILIYOUNGUZA NYUMBA WILAYANI
NYAMAGANA.
KWAMBA TAREHE
10.06.2017 MAJIRA YA SAA 18:30HRS KATIKA MTAA WA LUMUMBA KATA NA WILAYA YA
NYAMAGANA JIJI NA MKOA WA MWANZA, MADUHU MASUNGA LIGUSHI @ MZEE SHINYANGA,
MIAKA 75, MFANYABIASHARA NA MKAZI WA MTAA WA LUMUMBA, AMEFARIKI DUNIA KATIKA
AJALI YA MOTO ULIOUNGUZA NYUMBA YAKE KISHA KUJERUHI WATOTO WAKE WAWILI
WALIOFAHAMIKA KWA MAJINA YA 1.NGALULA MADUHU MIAKA 39, MFANYA BIASHARA NA MKAZI
WA MTAA WA LUMUMBA, 2.BRIAN MADUHU MIAKA 26, MKAZI WA MTAA WA LUMUMBA, NA
KUSABABISHA UHARIBIFU WA MALI NA VITU VILIVYOMO NDANI YA NYUMBA HIYO IKIWEMO
KIASI KIKUBWA CHA FEDHA AMBAZO HADI SASA THAMANI YAKE BADO HAIJAFAHAMIKA.
INASEMEKANA KUWA KABLA
YA AJALI HIYO YA MOTO KUTOKEA MAREHEMU ALIKUA NDANI YA NYUMBA YAKE YEYE PAMOJA
NA WATOTO WAKE, NDIPO GHAFLA MAJIRA TAJWA HAPO JUU ULIZUKA MOTO MKALI ULIOKUWA
UNAUNGUZA NYUMBA YAKE. INADAIWA KUWA KUTOKANA NA HALI HIYO MAREHEMU ALIKUWA
AKICHUKUA BAADHI YA MALI ZAKE NDANI ILI AWEZE KUTOKA NAZO NJE NDIPO KWA BAHATI
MBAYA MOTO ULIZIDI NA YEYE KUSHINDWA KUTOKA NJE NA KUPELEKEA KUUNGUA HUMO NDANI
NA BAADAE KUFARIKI DUNIA NA MALI ZAKE KUTEKETEA.
AIDHA MOTO HUO ULIWEZA
KUTHIBITIWA KWA KUSHIRIKIANA NA JESHI LA
POLISI, JESHI LA ZIMA MOTO NA UWOKOAJI PAMOJA NA TANESCO NA KUEPUSHA
KULETA MADHARA MAKUBWA KWA BAADHI YA MAJENGO MENGINE YA BIASHARA YALIYOPO ENEO
HILO. AIDHA MOTO HUO UNGEWEZA KUDHIBITI
MAPEMA LAKINI KUTOKANA NA MIUNDO MBINU YA ENEO HILO KUWA MIBOVU ILISHINDIKANA
KWANI KULIKUWA NA UKUTA MKUBWA NA KUPELEKEA MAGARI YA MAJI YA JESHI LA ZIMA
MOTO NA JESHI LA POLISI KUSHINDWA KUINGIA NA KUPELEKEA KUTOKEA KWA VIFO NA
UHARIBIFU WA MALI.
THAMANI YA MALI NA VITU
VILIVYOTEKETEA KATIKA AJALI HIYO YA MOTO BADO HAIJAFAHAMIKA, JESHI LA POLISI
PAMOJA NA JESHI LA ZIMA MOTO KWA KUSHIRIKIANA NA TANESCO WANAENDELEA KUFANYA
UCHUNGUZI NA UPELELEZI KUHUSIANA NA TUKIO HILO ILI KUJUA CHANZO CHA MOTO HUO, MAJERUHI
WAMEPELEKWA HOSPITALI YA MKOA YA SEKOU TOURE KWA AJILI YA MATIBABU NA HALI ZAO
ZINAENDELEA VIZURI, MWILI WA MAREHEMU UMEHIFADHIWA HOSPITALI YA RUFAA YA
BUGANDO KWA AJILI YA UCHUNGUZI PINDI UCHUNGUZI UKIKAMILIKA UTAKABIDHIWA KWA
NDUGU WA MAREHEMU KWA AJILI YA MAZISHI.
KAMANDA WA POLISI MKOA
WA MWANZA NAIBU KAMISHINA WA POLISI AHMED MSANGI ANATOA POLE KWA WANAFAMILIA WA
MAREHEMU, NDUGU, JAMAA NA MARAFIKI KWA MSIBA MZITO AMBAO UMEWAPATA MUNGU AWATIE
NGUVU NA UVUMILIVU KATIKA KIPINDI HIKI KIGUMU AMBACHO WANAPITIA, LAKINI PIA
ANAWAOMBEA MAJERUHI WAPONE HARAKA ILI WAWEZE KUENDELEA NA SHUGHULI ZAO KAMA
AWALI, AIDHA PIA ANAWAOMBA WANAFAMILIA KUWA WAVUMILIVU WAKATI HUU AMBAPO POLISI
WANAENDELEA NA UCHUNGUZI ILI KUWEZA KUFAHAMIKA CHANZO CHA AJALI HIYO YA MOTO.
AIDHA ANAWAOMBA WANANCHI KUWEKA MIUNDOMBINU MIZURI/RAFIKI KWENYE MAKAZI YAO
ITAKAYORUHUSU UOKOAJI WA VITU NA MALI PINDI ZINAPOTOKEA AJALI ZA AINA KAMA HII.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.