Mkaguzi
wa Polisi wa wilaya ya Korogwe, Merkiad Makumba akikata utepe wakati
wa kuzindua duka la Airtel katika wilaya ya Korogwe mkoani Tanga,
akishuhudia ni Afisa wa wateja wa Airtel Korogwe, Bi Elen na
Meneja mauzo wa Airtel Tanga, Habibu Kiango
Korogwe waishukuru Airtel kwa Kufungua duka la kisasa
Wakati uhalifu wa mtandao ukionekana kushika kasi duniani,Jamii
imetakiwa kuzitumia simu za mkononi katika kulisaidia jeshi la polisi
kubainisha watu wanaojihusisha na vitendo vya kihalifu kama sehemu ya
kutekeleza haki yao ya kikatiba.
Wito
huo ulitolewa na Mkaguzi wa Polisi Merkiad Makumba jana kwa niaba ya
Kamanda wa Polisi wa wilaya ya Korogwe , wakati akizindua duka la Kisasa
la kampuni ya simu za mkononi la
Airtel katika wilaya hiyo mkoani Tanga.
Hatua
hiyo itasaidia kukabiliana na vitendo vya namna hiyo ambavyo
vinahatarisha ustawi wa raia na mali zao…alisema Mkaguzi Makumba.
“
Wahalifu wengi wanatumia mawasiliano ya simu za mkononi na wamekuwa
wakiwasiliana nanyi,iwapo mtazitumia simu kwa nia njema Tanzania itakuwa
sehemu salama ya kuishi” alisema Mkaguzi
Mkumba
Meneja mauzo wa Airtel Tang, Habibu Kiango alisema duka hilo limewarahisishia wateja kupata huduma za Airtel kwa urahisi zaidi blia ya kwenda umbali mrefu kufuata huduma za mawasiliano . natoa wito kwa wakazi wa hapa na maeneo ya karibu kutumia fursa hii katika kukuza na kuendeleza biashara zao.
Meneja mauzo wa Airtel Tang, Habibu Kiango alisema duka hilo limewarahisishia wateja kupata huduma za Airtel kwa urahisi zaidi blia ya kwenda umbali mrefu kufuata huduma za mawasiliano . natoa wito kwa wakazi wa hapa na maeneo ya karibu kutumia fursa hii katika kukuza na kuendeleza biashara zao.
Kiango
aliongeza kwa kusema duka hili litatoa huduma nyingi pamoja na kusajili
line, kutoa huduma za kifedha za Airtel Money, kuunganisha wateja na
huduma za intaneti na nyingine
nyingi , aidha alitumia fursa hilo kuwakaribisha wakazi wa Korogwe
kulitembelea duka hilo.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.