Charles Munyaneza, Katibu Mtendaji
wa Tume Huru ya Uchaguzi amewaambia waandishi wa habari kwamba,
wanakadiria wasimamizi wa uchaguzi ujao watafikia 2000.
Amesema kuwa, miongoni mwa waangalizi
hao ambao wamewasilisha maombi ya kupewa vibali ni mabalozi wa mataifa
ya kigeni nchini humo na kwamba, wengine ni kutoka Jumuiya ya Afrika
Mashariki na waangalizi binafsi.
Hata hivyo, Umoja wa Ulaya tayari
umeshatangaza kuwa, hautatuma waangalizi wake nchini Rwanda. Wakati uo
huo, msemaji wa Mashirika ya kiraia nchini humo Jean-LĂ©onard Sekanyange,
amesema watatuma waangalizi zaidi ya 200 kushuhudia Uchaguzi huo.
Kampeni rasmi za uchaguzi huo,
zinatarajiwa kuanza tarehe 14 mwezi Julai na kumalizika Agosti tatu
ikiwa ni siku moja kabla ya kufanyika uchaguzi wenyewe..
Rais Paul Kagame hatarajiwi kupata upinzani mkali katika uchaguzi ujao.
Hayo yanajiri katika hali ambayo, jana Tume Huru ya Uchaguzi nchini
Rwanda ilipasisha majina mawili tu ya wagombea wa kiti cha Rais kutokana
na wagombea wengine wanne waliowasilisha fomu za kuwania nafasi hiyo
kutotimiza masharti.Rais Paul Kagame hatarajiwi kupata upinzani mkali katika uchaguzi ujao.
Waliopasishwa ni Rais Paul Kagame wa chama tawala cha RPF na Frank Habineza wa Democratic Green Party of Rwanda.
Kwa mujibu wa taarifa ya tume hiyo,
wagombea wanne ambao hawakupasishwa jana wana muda hadi kufikia Julai 6
mwezi ujao wawe wamekamilisha masharti vinginevyo ni wagombea wawili tu
watakaochuana katika kuwania kiti cha Urais katika uchaguzi ujao.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.