ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Tuesday, June 27, 2017

HOFU YA MAHARAMIA YAZIDI KUPANDA, MLIPUKO WA KUTISHA WATOKEA MELINI KATIKA PWANI YA PUNTLAND, SOMALIA.


Duru za habari nchini Somalia zimeripoti habari ya kutokea mripuko mkubwa ndani ya meli katika pwani ya Puntland, kaskazini mashariki mwa Somalia.
Ali Shire, meya wa bandari ya Alula, huko Puntland, amethibitisha habari hiyo na kusema kuwa, mripuko huo uliambatana na moto mkali ndani ya meli hiyo. 

Kwa mujibu wa afisa huyo, meli hiyo inaonekana kuwa ni mali ya jeshi kwa kuwa, baada ya mripuko huo zilikuja meli mbili nyingine za kijeshi za kigeni kwa ajili ya kuwaokoa watu waliokuwa ndani ya meli hiyo.

 
Maharamia wa Somali.
Hadi sasa haijafahamika mripuko huo umetokana na hitilafu ndani ya meli hiyo au ni shambulio. Bandari ya Alula inatajwa kuwa eneo linalotumiwa sana na mabaharia ambao huwa wanafanya vitendo vya uhalifu katika maji ya bahari ya Somalia. 

Wimbi la uharamia katika pwani ya Somalia linaonekana kuwa changamoto kubwa kwa meli za biashara zinazopita katika maji ya nchi hiyo. 

Mwezi April mwaka huu, mkuu wa ofisi ya Umoja wa Mataifa ya kupambana na mihadarati na uhalifu, Yury Fedotovo alitahadharisha kuhusu hatari, vitisho na mashambulizi ya maharamia wa baharini nchini Somalia na kuitaka jamii ya kimataifa ifanye juhudi kubwa zaidi za kupambana na maharamia hao.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.