Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran Mohammad Javad
Zarif amesema kuna haja ya kuwepo jukwaa la kustawisha mazungumzo baina
ya nchi za Ghuba ya Uajemi huku akitoa wito kwa nchi za eneo hili
kusitisha mashindano yao ya silaha.
Akizungumza mjini Berlin Ujerumani Jumatatu katika Baraza la
Sera za Kigeni la Ulaya, Zarif amesema mashindano ya silaha Mashariki ya
Kati yanatokana na uhusiano wa nchi za Magharibi na baadhi ya nchi za
eneo.Aidha Zarif ametoa wito kwa nchi za Ulaya kutumia ushawishi wao kupungua mzozo katika Ghuba ya Uajemi ambao umeibuka baada ya Saudi Arabia kuchochea waitifaki wake kukata uhusiano na nchi jirani ya Qatar.
Emir wa Qatar Sheikh Tamim Aal Thani
Saudi Arabia, Bahrain, Misri na Umoja wa Falme za Kiarabu
zimekata uhusiano wa kidiplomasia na Qatar na pia kuiwekea nchi hiyo
mzingiro wa nchi kavu, angani na baharini.
Nchi hizo zimedai kuwa Qatar
inaunga mkono ugaidi na kuvuruga uthabiti katika eneo madai ambayo wakuu
wa Doha wameyakanusha.
Zarif amesema nchi hizo ambazo zinaituhumu
Qatar kuunga mkono ugaidi pia zimetoa tuhuma hizo zisizo na msingi dhidi
ya Iran lengo likiwa ni kufunika kufeli kwao katika kukidhi mahitaji ya
watu wao.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.