Huku mgogoro ukiendelea kushtadi kati ya
Marekani na Korea Kaskazini, Rais Donald Trump wa Marekani amesema kuwa,
yupo tayari kukutana na kiongozi wa Korea Kaskazini, Kim Jong-un.
Trump ameyasema hayo katika
mahojiano na jarida la Bloomberg na kusema kuwa, ikiwa atakutana na
Kiongozi wa Korea Kaskazini, Kim Jong-un hiyo itakuwa fakhari kubwa
kwake. Amesisitiza kuwa, ikiwa kutaandaliwa mazingira kwa ajili ya
mkutano huo, yeye yupo tayari kabisa kukutana na kiongozi huyo kijana wa
Korea Kaskazini.
Rais Donald Trump ameongeza kuwa na
hapa ninamnukuu: “Wanasiasa wengi hawawezi kuzungumza matamshi kama
haya, lakini mimi ninasema wazi kwamba, nitakutana na Kim Jong-un ikiwa
kutaandaliwa mazingira.” Mwisho wa kunukuu. Rais Donald Trump wa
Marekani ametamka hayo katika hali ambayo, harakati za kijeshi za
Washington katika Peninsula ya Korea, zimeshadidisha mgogoro katika eneo
hilo kiasi cha kuifanya serikali ya Korea Kaskazini kuongeza harakati
zake za silaha za nyuklia na makombora ya balestiki kwa ajili ya
kukabiliana na vitisho hivyo vya Marekani.
Hii ni katika hali ambayo, kwa mara nyingine serikali ya Korea Kaskazini imeitahadharisha Marekani kwamba, ikiwa meli za kivita za nchi hiyo zitaendelea kukaribia maji yake katika Peninsula ya Korea, basi itaziangamiza silaha za nyuklia za Washington na kuzigeuza kuwa vyuma chakavu.
Hii ni katika hali ambayo, kwa mara nyingine serikali ya Korea Kaskazini imeitahadharisha Marekani kwamba, ikiwa meli za kivita za nchi hiyo zitaendelea kukaribia maji yake katika Peninsula ya Korea, basi itaziangamiza silaha za nyuklia za Washington na kuzigeuza kuwa vyuma chakavu.
Katika hatua nyingine, Pyongyang
imetangaza kuwa, katika kufuatilia siasa za uhasama za Marekani na
washirika wake, hususan Korea Kusini na Japana, imekusudia kujizatiti
kwa silaha za nyuklia ili isiweze kushambuliwa kama ilivyoshambuliwa
nchi ya Syria. Kwa mujibu wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Korea Kaskazini,
Pyongyang imeazimia kuunda kwa haraka sana silaha nyingi za nyuklia ili
kukabiliana na vitisho vya Marekani.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.