Wanachama wa genge la kigaidi na ukufurishaji la Daesh, wamewaua raia 10 katika mkoa wa Nainawa (Nineveh) nchini Iraq.
Shirika la Habari la Sumaria News
limeripoti kuwa, magaidi hao wameenedelea kutenda jinai dhidi ya
binaadamu nchini humo kwa kuwanyonga raia 10 ambao walikataa
kushirikiana nao. Kabla ya hapo pia wanachama wa kundi hilo waliwaua
raia wengine 50 huko magharibi mwa mji wa Mosul kwa kosa hilo hilo.
Tangu genge hilo liudhibiti mji wa Mosul
mwaka 2014, limewanyonga karibu raia 1000 wa mji huo. Habari nyingine
ni kwamba, kundi hilo maarufu kwa kutenda jinai dhidi ya binaadamu,
limeharibu maktaba ya chuo kikuu cha mji wa Mosul iliyokuwa na hadhi ya
kimataifa na maarufu sana ambayo ilikuwa na zaidi ya vitabu laki moja na
iliyosajiliwa na Shirika la Elimu, Sayansi na Utamaduni la Umoja wa
Mataifa (UNESCO).
Awali maktaba hiyo ilishambuliwa na
ndege za kivita za Marekani kwa kisingizio cha kupambana na wanachama wa
kundi hilo ambao walikuwa wamekidhibiti chuo hicho, hujuma ambayo
ilisababisha uharibifu mkubwa. Chuo kikuu hicho kilikuwa kinahesabika
kuwa kitivo cha pili cha kielimu nchini Iraq.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.