ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Saturday, May 27, 2017

MSUMENO WA KICHUYA WAI-CHANACHANA MBAO


Makali ya msumeno wa Shiza Kichuya jioni ya leo ndiyo yamefanikiwa 'kuzichana chana' mbao za Mbao FC toka Mwanza na hata kuipa Simba ubingwa wa Azam Federation Cuf katika dimba la Jamhuri mjini Dodoma.

Wakati timu hizo zikiwa sare ya 1-1 hadi dakika ya 118, Simba ikapata penati baada ya beki mmoja wa Mbao Fc kuunawa mpira katika harakati za kuokoa mpira usitinge nyavuni.

Kichuya alipiga penati hiyo kiufundi akimwacha mlinda mlango wa Mbao Fc akienda kushoto naye akiutupia kulia.

Kiungo wa Simba, James Kotei amekuwa mchezaji bora wa mechi ya fainali ya Kombe la Shirikisho. Katika mechi hiyo, Simba imeshinda kwa mabao 2-1 na kubeba ubingwa. Kotei alicheza namba nne na kuonyesha kiwango cha juu kabisa katika mchezo huo.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.