Mbunge wa Jimbo la Hai, Freeman Mbowe, amejibu swali la Rais John Pombe
Magufuli, aliyehoji matumizi ya Sh1.3 bilioni za mfuko wa barabara kwa
mwaka wa fedha 2016/2017 katika wilaya hiyo.
Aprili 29 akihutubia mkutano wa hadhara katika mji wa Bomang’ombe, Rais
alihoji matumizi ya fedha hizo, baada ya Mwenyekiti wa Halmashauri ya
Hai, Helga Mchomvu kumkumbusha ahadi yake ya barabara.
Akiwa katika kampeni za uchaguzi mkuu 2015, Rais Magufuli aliwaahidi
wananchi wa Jimbo la Hai barabara ya lami yenye urefu wa kilometa tano,
hivyo Mchomvu akamkumbusha juu ya ahadi hiyo.
Hata hivyo, Rais hakujibu moja kwa moja juu ya ombi hilo, bali alihoji
matumizi ya Sh1.3 bilioni za mfuko wa barabara na na kuahidi kumtuma
Waziri wa Tamisemi, kuchunguza matumizi yake.
Lakini juzi akiwa katika harambee kuchangia ujenzi wa madarasa ya Shule
ya Msingi Kambi ya Raha, Mbowe alisema kiasi ambacho kimepokelewa na
halmashauri ni Sh300 milioni na siyo Sh1.3 bilioni.
“Wakati wa ziara Rais aliuliza kiasi ambacho tumekwishapatiwa kwa ajili
ya ukarabati wa barabara lakini kwa bahati mbaya waliompatia taarifa
wakampatia taarifa isiyo sahihi,”alisema Mbowe.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.