ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Sunday, May 7, 2017

MAMA SAMIA SULUHU KUONGOZA MAELFU YA WAOMBOLEZAJI KESHO KATIKA KUAGA MIILI YA MAREHEMU


 

Serikali kugharamia Msiba wa Arusha


Serikali ya Jamhuri wa Muungano wa Tanzania imegharamia Sanda pamoja na majeneza kwa ajili ya Wanafunzi wa Shule ya Lucky Vicent waliopoteza maisha mapema jana kwenye ajali iliyokuwa ikihusisha safari ya kimasomo.

Akitoa taarifa hiyo leo Meya wa Jiji la Arusha , Mh. Calist Lazaro amesema kuwa taarifa za awali zinaonyesha kuwa tayari Serikali imekwishalipia gharama za majeneza na sanda ya kuhifadhia miili ya marehemu ambao kesho wanatarajiwa kufanyiwa ibada katika Uwanja wa mpira wa Sheikh Amri Abeid.

Aidha, Mh. Lazaro amesema kuwa viongozi mbali mbali wakiwemo mawaziri pamoja na wabunge bado wanaendelea kukusanyika katika eneo la shule ya Lucky Vicent  kwa ajili ya kikao na baadae majira ya saa tisa au kumi taarifa rasmi ya serikali itatolewa na Mkuu wa Mkoa wa Arusha.

Kuhusu kiongozi gani atakayeongoza maelfu ya waombolezaji hiyo kesho Jembe Fm 93.7 inaungana na mwanahabari wake aliyeko mjini Arusha Woindeshizza naye huyu hapa.BOFYA PLAY KUSIKILIZA
WAKATI HUO HUO.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu, Akizungumza Jambo na Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mrisho Gambo mara baada ya kuwasili katika uwanja wa KIA.


Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Samia Suluhu Hassan amewasili mjini Arusha jioni hii ambapo hapo kesho ataongoza wananchi wa mkoa wa Arusha na mikoa ya jirani katika kuaga miili ya wanafunzi 32,walimu Wawili pamoja na dereva Mmoja wa shule ya Lucky Visent iliyopo Jijini Arusha waliopata ajali jana tarehe 06-May-2017 katika eneo la Rhotia wilayani Karatu mkoani Arusha.

Wanafunzi na walimu hao walipata ajali hiyo wakati wanaenda kwenye shule  iitwayo Tumaini kwa ajili ya kufanya mitihani wa ujirani mwema baada ya gari walilokuwa wakisafiria kuacha njia na kutumbukia korongoni kwenye eneo la Rhotia wilayani Karatu.

Ibada na dua za kuaga miili ya marehemu hao itafanyika katika uwanja wa Sheikh Amri Abeid Jijini Arusha kuanzia Saa Mbili asubuhi hapo kesho.

Katika uwanja wa ndege wa Arusha Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Samia Suluhu Hassan na ujumbe wake wamepokelewa na Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe Mrisho Gambo pamoja na Viongozi wa wengine wa mkoa huo.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.