Mkuu wa shule ya Shule ya sekondari ya Vianzi Ashura Manaki ( wa pili kulia ) kaifatiwa na pamoja na Meneja Huduma kwa Jamii wa Airtel, Bi Hawa Bayumi (wapili kushoto) na Meneja Mauzo wa Airtel Pwani, Philipi Nkupuma kwa pamoja wakionyesha vitabu vya sayansi mara baada ya Airtel kukabidhi vitabu hivyo kwa shule ya sekondari ya Vianzi pindi walipotembelea shuleni hapo
. Meneja
Huduma kwa Jamii wa Airtel, Bi Hawa Bayumi akimkabidhi vitabu vya
sayansi mwalimu mkuu wa shule ya sekondari ya Vianzi Bi Ashura Manaki
wakati Airtel ilipotembelea shule
hiyo kutoa msaada wa vitabu vya taaluma . akishuhusia ni Zamda Said ni
Mwenyekiti wa Bodi ya Shule
Press Release
Airtel yatoa msaada wa vitabu vya sayansi kwa shule ya sekondari Vianzi
Suala
la uhaba wa vitabu vya masomo ya Sayansi, maabara pamoja na walimu wa
masomo hayo limekuwa likisababisha baadhi ya wananfunzi kushindwa kumudu
na hivyo kuyaepuka masomo hayo,licha ya serikali na wadau mbalimbali
kuhamasisha wanafunzi kuchukua masomo hayo.
Kutokana
na hali hiyo Kampuni ya Simu za Mkononi ya Airtel imetoa msaada wa
Vitabu vya Masomo ya Sayansi vyenye thamani ya Shilingi Milioni Tatu
katika Shule ya Sekondari Vianzi iliyopo Mkuranga Mkoani Pwani ambayo
ina zaidi ya wanafunzi 400 ikiwa na walimu watatu kwa masomo yote ya
Sayansi (biolojia, fizikia, kemia na hesabu). Hatua hiyo ni mwendelezo
wa Kampuni hiyo kusaidia katika elimu shule mbalimbali hapa nchini ili
kuinua kiwango cha elimu katika masomo ya Sayansi.
Mkuu
wa Shule ya Sekondari Vianzi Mwl. Ashura Manaki amesema kuwa shule yake
imekuwa ikikabiliwa na changamoto ya ukosefu wa walimu, maabara za
kutosha pamoja na vitabu hali ambayo imekuwa ikisababisha wanafunzi
kukimbia masomo ya Sayansi.
“Tunaishukuru
sana Airtel kwa msaada huu wa vitabu ebu fikilia tuna upungufu wa
walimu,sasa likija tatizo la ukosefu wa vitabu unadhani wanafunzi
watayapenda masomo ya sayansi,lakini kwa sasa nina matumaini tutaweza
kusonga mbele,”alisema Manaki.
Kwa
upande wa Meneja wa Huduma kwa Jamii kutoka Airtel Hawa Bayumi ameleeza
kuwa licha ya Kampuni hiyo kujikita katika mambo mbalimbali ya Kijamii
wameona umuhimu wa kuisaidia shule hiyo ambayo inachangamoto ya walimu
wa sayansi lakini wakakuta hata vitabu navyo ni changamoto wakaamua
kutoa msaadahuo.
”Licha
ya Airtel kusaidia mambo mbalimbali ya kijamii tumeona kuna umuhimu
mkubwa kuisaidia vitabu vya sayansi shule hii kutokana na kukabiliwa na
changamoto ya uhaba wa walimu wa sayansi pamoja na vitabu vya sayansi
tuna matumaini vitaweza kusaidia shule hii kujenga wataalamu wa sayansi
hasa ukizingatia serikali inaweka juhudi kufikia Tanzania ya viwanda ni
muhimu kuwekeza katika rasilimali watu na kujenga watanzania weny
weledi. Lengo letu ni kuendelea kuwezesha vijana kufikia malengo yao
kupitie elimu na ujasiriamali,”alisema Bayumi.
Zamda
Said ni Mwenyekiti wa Bodi ya Shule hiyo amesema kuwa shule hiyo bado
ina mahitaji ya walimu wa sayansi lakini kwa kupatiwa vitabu hivyo
vitasadia hata wanafunzi kuweza kujisomea huku akiwaasa wanafunzi
kutumia fursa hiyo kufaulu masomo ya sayansi.
“Ni
kweli tatizo la uhaba wa walimu pamoja na ukosefu wa vifaa vya
kujifunzia na kufundishia ni changamoto kwa shule hii lakini nawaombeni
wanafunzi kutumia fursa hii kuweza kujisomea maana vitabu gharama yake
ni kubwa,”alisema Said
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.