Wednesday, April 19, 2017
HABARI
Rais Donald Trump wa Marekani ameiagiza kamisheni
ya usalama wa taifa ya nchi hiyo kuangalia upya makubaliano kwa jina la
Mpango Kamili wa Pamoja wa Utekelezaji (JCPOA).
Rex Tillerson Waziri wa Mashauri ya Kigeni wa Marekani amesema
kuwa Trump ameitaka kamisheni ya usalama wa taifa ya nchi hiyo ichunguze
iwapo hatua ya Rais msaafu wa nchi hiyo Barack Obama ya kuifutia
vikwazo Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ilikuwa kwa maslahi ya Washington au
la. Itakumbukwa kuwa akiwa katika kampeni za uchaguzi wa rais mwaka
jana, Trump aliyataja makubaliano ya JCPOA kuwa ni maafa na makubaliano
mabaya zaidi kuwahi kufikiwa duniani na kuahidi kuwa, angeyachana katika
siku yake ya kwanza ya kuanza kazi huko White House.
Jamii ya kimataifa ukiwemo Umoja wa Ulaya zimekiri kuwa Jamhuri ya
Kiislamu ya Iran imetekeleza ahadi zake zote katika fremu ya makubaliano
hayo, hata hivyo Marekani imekuwa ikifanya kila linalowezekana
kukwamisha makubaliano hayo ya kimataifa. Federica Mogherini Mkuu wa
Siasa za Nje wa Umoja wa Ulaya hivi karibuni naye alisisitiza kuwa
makubaliano ya JCPOA ni milki ya jumuiya za kimataifa na kwamba si
makubaliano ambayo yanaweza kuratibiwa na pande mbili tu na kufanyiwa
mabadliko na pande hizo.
Federica Mogherini, Mkuu wa Siasa za Nje wa Umoja wa Ulaya
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.