Jiji la Mwanza. |
NA ANNASTAZIA
MAGINGA,Mwanza
MAMLAKA ya Majisafi na
Usafi wa Mazingira Mkoa wa Mwanza imesema inazidai taasisi za umma Sh bilioni
mbili huku wateja wa kawaida wakidaiwa Sh million 300
Akizungumza na G sengo Blog
Kaimu Afisa Habari wa Mamlaka hiyo Oscar Twakazi kwa niaba ya Mkurugenzi
Mhandisi Antony Sanga amesema wanatekeleza agizo la Rais Dk. John Pombe
Magufuli la kusitisha utoaji wa huduma kwa wadaiwa sugu wa ankara za
maji zikiwamo taasisi za umma na binafsi.
Twakazi amesema kuhusu wateja ambao wapo katika daraja la
kawaida, tayari wameikabidhi kampuni ya Sai Soliciators & Avocates
majina ya waidaiwa wote ili kukuksanya fedha hizo kabla ya
kufikia uamuzi wa kusitisha huduma kwao.
“Hapa kuna wateja wetu aina
tatu, wateja wa kaiwada, kampuni na viwanda sambamba na taasisi za umma, sasa
kwa upande wa wateja wa kawaida tunawadai Sh milioni 300 ambazo zitakusanywa na
Sai Soliciators & Avocates.
“Kwa upande wa kampuni na
viwanda hatuna shida nao maana ni walipaji wazuri, tatizo lipo kwenye taasisi
za umma Mpaka sasa Mwauwasa inawadai Sh bilioni 2, tunatarajia
kuwapo kwa ‘notes’ ya kulipa madeni yao, lakini tumewasiliana na hazina
makao makuu juu ya madeni yao na wametuelekeza kwamba tuhakikishe madeni hayo
upya na kuwapelekea wao ili waweze kuingiza fedha hizo moja kwa moja kwetu,”amesema.
Twakazi amesema kwamba baada ya kufanya mawasiliano na hazina,
wamebaini kuwa taasisi za umma ambazo zinadaiwa na Mwauwasa zilikuwa zikipewa
fedha lakini hazikuona umumhimu wakulipa badala yake walizitumia kwa
mambo mengine ambayo waliyaona ni kipaumbele kwao.
Akizungumzia tatizo
lilitokeza takribani wiki mfululizo la kutokuwapo kwa uhakika wa maji jijini
Mwanza, amesema lilitokana na hitilifafu ya umeme iliyojitokeza
kwenye kituo kikuu cha kuzalishaji maji eneo la Kapri point.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.