KUFUATIA kuwepo kwa madeni
ya ankra ya maji kwa taasisi za umma Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Mwanza
(Mwauwasa) imesema inajipanga kununua mashine maalumu za luku
ambazo zitafungwa kwenye taasisi za umma zilizounganishiwa huduma ya maji ili
kuepuka madeni.
Mamlaka hiyo imesema lengo
la mashine hizo ni kudhibiti na kuepuka madeni ya taasisi za umma ambazo
zimekuwa zikitumia maji mengi huku zikishindwa kulipa ankara jambo ambalo
linasababisha Mwauwasa kushindwa kujiendesha na kufikia malengo ya kila mwaka.
Akizungumza na G sengo blog Kaimu
Afisa Habari na Mawasiliano wa Mwauwasa, Oscar Twakazi kwa niaba
ya Mkurugenzi wa mamlaka hiyo, Mhandisi Antony Sanga, ambapo
ameeleza kuwa licha ya mpango huo kuanza na wateja wakubwa ambao wamekuwa
wasumbufu katika ulipaji wa ada za maji lakini pia utawahusisha wananchi.
Amesema mpango huo unatarajia
kuanza mwaka wa fedha ujao 2017/2018 ili kuweka mfumo unaojulikana kwa jina la “malipo
kabla ya matumizi”,utakao saidia kumbana mtumiaji wa maji kwa kununua kila
anapohitaji.
Twakazi amesema mfumo huo
utakawa suluhisho kwa taasisi za umma ambazo zimezoea kutumia maji mengi ya
mamlaka bila kulipa ankara na hata wanapotengewa fedha kutoka
hazina, huzitumia kwa mambo mengine.
“Hizi taasisi za umma
tunazidai Sh bilioni mbili ikilinganishwa na Sh milioni 300 za wateja wa
kawaida, tumekaa na kuona tukija na mfumo wa malipo kabla ya matumizi tutakuwa
tumekomesha suala la taasisi hizi kutolipa ankara za maji.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.