RAIS Jacob Zuma wa Afrika Kusini leo
ameyataja maandamano ya wiki iliyopita nchini humo ya kumshinikiza
ajiuzulu kuwa ni ya kibaguzi.
Makumi
ya maelfu ya wananchi Ijumaa iliyopita waliandamana katika miji
mbalimbali ya Afrika Kusini kudhihirisha hasira zao kutokana na kashfa
mbalimbali za ubadhirifu, ukosefu wa ajira na kuzorota uchumi chini ya
utawala wa Rais Zuma. Hatua ya Zuma ya kumfuta kazi Pravin Gordhan
Waziri wa Fedha wa Afrika Kusini aliyekuwa akiheshimika nchini humo
imeibua upinzani na malalamiko mapya ya wananchi na kutoka kwa shakhsia
wa ngazi ya juu wa chama tawala ANC, akiwemo Makamu wa Rais.
Rais Jacob Zuma amesema kuwa maandamano ya wiki iliyopita
yamedhihirisha kuwa ubaguzi upo huko Afrika Kusini.
Amesema mabango na
maberamu yaliyobebwa na waandamanaji yalidhihirisha imani ambazo amesema
walidhani zilishatokomezwa, huku mabango mengine yakiwa yamechorwa raia
weusi na kuwaonyesha kuwa ni nyani.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.