RAIS John Pombe Magufuli wa Tanzania leo Alkhamisi amefanya mabadiliko mengine katika Baraza la Mawaziri.
Taarifa
ya Ikulu ya Tanzania imesema kuwa, katika mabadiliko hayo, Rais
Magufuli amemteua Dk Harrison George Mwakyembe kuwa Waziri wa Habari,
Utamaduni
Sanaa na Michezo, nafasi iliyokuwa ikishikiliwa na kada maarufu wa
chama tawala cha CCM, Nape Nnuaye. Kwa mujibu wa taarifa hiyo,
mabadiliko mengine yaliyofanywa leo na Rais wa Tanzania ni kumteua
Profesa Palamagamba Kabudi kuwa Waziri wa Katiba na Sheria.
Hata
hivyo taarifa hiyo ya Ikulu ya Tanzania haikutaja hatima ya waziri wa
zamani wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo, Nape Nnauye, bali imesema
tu kuwa uteuzi huo unaaza mara moja na wateule hao wawili wataapishwa
kesho Ijumaa mchana Ikulu jijini Dar es Salaam.
Rais John Pombe Magufuli wa Tanzania
Rais John Pombe Magufuli wa Tanzania
Ikumbukwe
kuwa jana Nape Nnauye alipokea ripoti ya tume aliyounda kwa ajili ya
kuchunguza uvamizi uliofanywa na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul
Makonda, katika majengo ya Clouds Media Group, uvamizi ambao
umelalamikiwa vikali na duru mbalimbali hususan vyombo vya habari vya
Tanzania.
Baada
ya kupokea ripoti hiyo yenye mapendekezo kadhaa mazito, Nnauye alisema
ataiwasilisha kwa wakubwa wake, Rais, Makamu wa Rais na Waziri Mkuu wa
Tanzania kwa ajili ya kuchukuliwa maamuzi.
Miongoni mwa mapendekezo ya tume hiyo ni pamoja na Waziri Nape Nnauye awasilishe rasmi malalamiko ya tasnia ya habari dhidi ya Makonda.
Miongoni mwa mapendekezo ya tume hiyo ni pamoja na Waziri Nape Nnauye awasilishe rasmi malalamiko ya tasnia ya habari dhidi ya Makonda.
Vyombo
vya dola viwachunguze askari walioingia na bunduki kwenye kituo cha
televisheni pamoja na kampuni ya Clouds Media kupitia upya miongozo,
kanuni, sheria na taratibu ili kudhibiti watu wasiohusika kuingia kwenye
chumba cha habari.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.