ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Thursday, March 2, 2017

MVUA YA MAWE YANYESHA LEO MWANZA.

Mvua kubwa iliyonyesha leo alasili jijini Mwanza na moja ya madhara yake katika barabara ya lami ya Kilimahewa mwanzoni toka barabara ya Makongoro - Airport, imesababisha moja ya miti kandokando mwa barabara hiyo kuanguka na kufunga barabara.
Hii siyo sukari wala chumvi wandugu, mvua iliyonyesha ikiambatana na mawe ndani ya muda mchache jijini Mwanza na wilaya zake imezalisha mabonge ya barafu na hii hapa ni matokeo yake... Maeneo yote ya kata za Nyamagana na kata za Mirongo mashuhuda wameripoti kuishuhudia hali hiyo.

Nako wilayani Ilemela maeneo ya Pasiansi, Kirumba, Kiloleli hadi Airport nako kumeripotiwa mvua hiyo.
Ze mti iz dauni.
Madharahata mtaroni.
Si miundombinu ya barabara pekee bali pia nguzo za umeme nazo hali tete kama picha inavyoainisha.
Mnara wa mawasiliano umeangukia paa la nyumba eneo la Kilimahewa.
Mafundi wakikarabati bati lililopata mushker na baada ya kuangukiwa na mnara.
Juu ya paa.
Muonekano mwingine kwa mtaa wa Kilimahewa.
Blogu hii inaendelea kufanya uchunguzi kubaini hasara na madhara yaliyo jitokeza mara baada yamvua hiyo kunyesha.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.