Mtu huyo aliyetambulika kwa jina la Steven Bahati anayekadiriwa kuwa na umri wa miaka 54 hadi56 amepatikana ikiwa siku ya 2 tangu kuzama kwake.
Filipo Muhota ni kijana aliyeshiriki kuusaka mwili huo anasema iliwalazimu kutumia mbinu ya kutega nyavu katika sehemu aliyozama jamaa huyo ili kuweza kuuopoa kwa haraka mwili huo ambao jana waliusaka tangu saa mbili asubuhi majira ya saa 2 mpaka jua lilipo zama wakiambulia patupu. BOFYA PLAY UMSIKILIZE AKISIMULIA
LEO majira hayo ya saa 6 mchana hatimaye mara baada ya kuhisi uzito mkubwa toka katika nyavu walizotega iliwalazimu kuzivuta nyavu hizo juu ndipo wakaona kitu kikubwa naam wakaamini sasa zoezi lao limezaa matunda.
Taratibu za kuusitiri mwili wa Marehemu Steven Bahati baada ya kunaswa na nyavu.
Sasa tayari kwa kuutoa majini.
Wadau wa habari toka Jembe Fm mbele Adolf Nzwala na Johari Ngassa macho mbele kuelekea kwenye ufukwe wakati wa kuunasua mwili wa mvuvi huyo aliyekufa maji.
Kushoto ni Mwenyekiti wa mtaa wa Soko Jumanne Madirisha amesema kuwa baada ya kuunasua mwili huo walitoa taarifa kwa jeshi la polisi kwaajili ya kutoa nafasi kwa jeshi hilo kufika eneo la tukio na kufanya uchunguzi wake kisha kutoka na ripoti ya tukio kwaajili ya taratibu nyingine.
Wananchi wa mtaa wa Soko katika eneo la tukio.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.