Wakulima
na wafugaji wa kata ya Nkiniziwa ,
Nzega wanufaika na huduma za mawasiliano za Airtel
- Kufatia uzinduzi wa minara ya mawasiliano katika kata za Mwakashahala. Kahamanhalanga, Songambele Itumba mkoani Tabora
- Takribani wakazi elfu 32 katika vijiji 6 kufurahia huduma na bidhaa za Airtel
Tabora,
Jumatano 15th March 2017,
wakulima na wafugaji wa kijiji cha Ngukumo kata ya Nkiniziwa wilaya ya Nzega mkoani Tabora wameipongeza Airtel kwa
kuwezesha upatikanaji wa huduma za mawasiliano ya uhakika na kuwawezesha kuangalia
bei za bidhaa na kutafuta masoko kupitia simu zao za mkononi
Hayo
yalisemwa na wakazi wa kijiji cha Ngukumo wakati wa uzinduzi huduma za
mawasiliano utakaowawezesha wakazi zaidi ya elfu 32 kutoka katika vijiji 6 kupata huduma za mawasiliano baada ya Airtel
kuwasha minara ya mawasiliano katika
maeneo ya Mwakashahalala Kahamanhalanga, Songambele Itumba mkoani hapo
‘’Tumekuwa tukipata changamoto nyingi sana ikiwemo
mawasiiano hafifu ambapo ilibidi kusafiri umbali mrefu kupata huduma za
mawasiliano, Tunaishukur kampuni ya Airtel kwa kuona ni vyema kutufikishia
huduma za mawasiliano hapa na kutuunganisha na ndugu jamaa na wafanyabiashara katika maeneo mbalimbali ndani na nje ya
nchi alisema mkazi wa kata ya Nkiniziwa, John
Akiongea
wakati wa uzinduzi, Mkuu wa Wilaya ya Nzega, Godfrey Ngupula alitambua na kupongeza juhudi zinazo fanya na
Airtel katika kuhakikisha huduma za mawasiliano zinapatikana kwa wote kufatia
mchango wake muhimu katika kukuza uchumi wa nchi na kusema ni muhimu kuwa na
mawasilino bora kwani kichocheo kikubwa katika kuboresha maisha ya watanzania
na kurahisisha shughuli zao za kijamaa na kiuchumi.
“naamini
mawasialiano haya yataweesha biashara katika wilaya hii kukua, na wakulima
watanufaika na huduma mbalimbali za simu zitakazowawezesha kutafuta masoko ya
bidhaa zao, kuangalia bei ya mazao, lakini pia watatumia huduma ya Airtel Money
kwaajili ya kufanya malipo na manunuzi kwa njia ya simu. Nawaasa wakazi wa
wilaya ya Nzega kutumia mawasiliano haya vyema na kuboresha maisha yao”
aliongeza Ngupula
Kwa upande wake Meneja wa Airtel mkoa wa
Tabora, Phidelis Lugangila alisema
“Airtel imejipanga kutoa huduma bora na za uhakika na kuwaomba wakazi wa kijiji
cha Ngukumo na vijiji vya jirani kutumia huduma na bidhaa za Airtel kupata kipato kupitia huduma zetu kama vile Airtel Money
kwa kuwa mawakala na kupata kamisheni kila mwezi na vilevile kutengeneza ajira
kwa vijana wengi.
Wakazi
wa mwashala wanajishughulisha zaidi na kilimo cha mahindi,pamba ,Karanga na Mpunga pamoja na
ufugaji
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.