SERIKALI ya Burundi imetangaza kuwa watu 700
wameaga dunia kutokana na ugonjwa wa malaria katika kipindi cha miezi
miwili iliyopita nchini humo.
Mabadiliko ya tabianchi na umasikini wa kupindukia unaowakabili watu wengi wa nchi hiyo vimetajwa kuwa sababu ya vifo hivyo.Waziri wa Afya nchini Burundi, Dakta Josiane Nijimbere amesema tangu Januari Mosi hadi Machi 10 mwaka huu, watu zaidi ya milioni moja na laki nane wameambukizwa malaria, ambapo 700 miongoni mwao wamepoteza maisha, sawa na takriban watu 10 kila siku.
Waziri wa Afya nchini Burundi, Dakta Josiane Nijimbere |
Maginwja ya kipindupindu na malaria yameenea sana kipindi hiki katika
nchi za Afrika. Oktoba mwaka jana, watu karibu 50 waliaga dunia ndani
ya siku 30 katika jimbo la Sokoto, kaskazini magharibi mwa Nigeria
kutokana na malaria.
Mwaka jana Shirika la Afya Duniani (WHO) lilitangaza kuwa, kuna uwezekano ugonjwa wa malaria utaangamizwa kabisa katika nchi sita za Afrika zinazosumbuliwa sana na maradhi hayo ifikapo mwaka 2020.
Mwaka jana Shirika la Afya Duniani (WHO) lilitangaza kuwa, kuna uwezekano ugonjwa wa malaria utaangamizwa kabisa katika nchi sita za Afrika zinazosumbuliwa sana na maradhi hayo ifikapo mwaka 2020.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.