ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Sunday, February 26, 2017

 SERIKALI YAWATAKA WANANCHI KUANZISHA DESTURI YA KUNUNUA KAZI ZA WASANII

Katibu Mkuu Wizara ya Habari,Vijana,Utamaduni na Michezo Prof Elisante Ole Gabriel akitoa ufafanuzi.

Katibu Mkuu Wizara ya Habari,Vijana,Utamaduni na Michezo Prof Elisante Ole Gabriel akisalimiana na baadhi ya wasanii waliojumuika kwenye kusanyiko hilo la faida.

Salaam salaam.

Picha ya pamoja.

Sisi.

Salaam.

Fredy Ngimba, mwanzilishi wa Afro Premiere.


Prof Elisante Ole Gabriel akiweka sahihi yake kwenye ubao maalum uliokuwepo kwenye uzinduzi wa Afro Premiere kama ahadi kuwa atanununua kazi za wasanii.

Prof Elisante Ole Gabriel kwenye picha ya pamoja na wasanii waliokuwa wamealikwa, wakiwemo Joh Makini na Nick wa Pili.
Serikali imewataka wananchi kuanzisha desturi ya kununua kazi za wasanii, kwakuwa ndiyo njia pekee inayoweza kuwanufaisha kwa kazi wanazozifanya.

Wito huo umetolewa wiki hii na Katibu Mkuu Wizara ya Habari,Vijana,Utamaduni na Michezo Prof Elisante Ole Gabriel wakati akizungumza kwenye uzinduzi wa tovuti a Afro Premiere, iliyoanzishwa kwa lengo la kuuza video za muziki za wasanii.

Alisema mpango huo unaweza kuwa ni moja ya mikakati muhimu ya kupambana na wezi wa kazi za wasanii, kwakuwa video za muziki zitakuwa zikipatikana kwenye mtandao huo peke yake kwa kipindi maalum na hivyo kuingiza pesa zinazoenda kwa msanii, serikali na watayarishaji moja kwa moja.

Pia alidai kuwa kwakuwa Afro Premiere itakuwa ikiweka nyimbo za Kiswahili zaidi, itasaidia kukikuza zaidi Kiswahili, ambacho ni cha 10 kati ya lugha elfu sita duniani na kuahidi kupitia wizara ya mambo ya nje, wizara yake itawaunganisha na Watanzania waliopo nje ya nchi.

Prof Ole Gabriel amewataka wasanii wao wenyewe kuunga mkono mpango huo sababu ndio njia pekee ya kuufanya ufanikiwe.
“Mpango huu utafanikiwa kama ninyi mkiwa sehemu ya mpango huu, kama ninyi wenyewe tena mkianza kuwa na kona kona na kuupiga vita, basi mpango huu utaonekana feki na utashindikana,” alisema.

Hadi sasa kuna video mbili mpya zilizowekwa kwenye Afro Premiere ambazo ni Go Low ya G-Nako na Jux pamoja na K wa Roma na Baghdad. Mashabiki wanaweza kununua nyimbo hizo kwa shilingi 300 tu kwa kutumia simu zao.

Kuiona video ya Go Low, bofya link hii>>> http://afropremiere.com/previd eo/1487839158_afropremiere.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.