Mwambusi amesema kuumia kwa Kamusoko kuliwafanya Simba waje zaidi katika eneo la katikati, jambo ambalo liliwasaidia kupitisha mipira kirahisi na hatimaye kuweza kupata mabao mawili na kuibuka na ushindi.
Amesema licha ya kumuigiza Said Makapu kuchukua nafasi ya Kamusoko, lakini hakufanya kazi ipasavyo, na pia anapungukiwa baadhi ya vitu alivyonavyo Kamusoko ikiwa ni pamoja na kuwa na maono pamoja na kuunganisha safu ya nyuma na mbele.
Sababu nyingine aliyoitaja Mwambusi ni umakini wa wachezaji wote kwenye timu yake kupungua na kushindwa kukaba, jambo lililofanya wawe wanakaba kwa macho.
"Wao Simba waliongeza namba katikati, sasa na sisi vijana wetu tuliowaingiza baada ya kamusoko kuumia walipaswa walitakiwa kuongeza namba katikati lakini wakashindwa,.... Pia umakini wa ukabaji kwa wachezaji wetu haukuwa mzuri, Simba walikuwa wanakuja wanapita watu wanawasindikiza kwa macho" - Amesema Juma Mwambusi.
Hata hivyo amesema matokeo hayo inagawa yanawaumiza, hayajawapotezea lengo lao la kutwaa ubingwa wa ligi kuu Tanzania na kwamba atakaa na walimu wenzake kurekebisha makosa ambayo yamejitokeza ili yasijirudie tena.
Katika mchezo huo, mabao ya Simba yalifungwa na Mavugo na Kichuya kipindi cha pili, huku la Yanga likifungwa na Msuva kwa njia ya penati, katika dakika ya 5
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.