ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Sunday, February 26, 2017

BAADA YA PEPSI KOMBE LA MEYA SASA MBUNGE WA NYAMAGANA ANAKUJA NA 'JIMBO CUP'



MAANDALIZI ya STANSLAUS MABULA MBUNGE CUP 2017 mashindano yatakayoanza hivi karibuni msimu wa mwaka 2017-2018 tayari yamekwishaanza.

Mapema wiki hii Mbunge wa Jimbo la Nyamagana Mhe. Stanslaus Mabula akiwa ameongozana na Naibu Meya wa Jiji la Mwanza Mhe. Bhku Kotecha wamekagua viwanja mbalimbali vya mashindano hayo ukiwemo uwanja wa Shule ya Msingi Milongo.

Kwa mujibu wa Mhe. Mabula amesema kuwa mashindano hayo yatatumia viwanja vitatu yaani Uwanja wa Shule ya Msingi Milongo, Uwanja mpya wa kisasa wa Nyamagana na Mkolani.

Mashindano hayo yanakuja ikiwa ni jitihada za Stanslaus Mabula katika kuwafungulia fursa vijana kupitia soka kama ilivyokuwa ada yake katika miongo kadhaa iliyopita wakati akiwa Mstahiki Meya wa Jiji La Mwanza ambapo aliwakutanisha vijana katika mashindano yaliyokuwa ya aina yake PEPSI KOMBE LA MEYA na washindi iliondoka na mtaji wa fedha taslimu pamoja na nyenzo mbalimbali za uwekezaji katika ujasiliamali kama vile bajaji ya mizigo ya magurudumu matatu na kadhalika.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.