Sherehe hiyo ya marudio imeandaliwa katika bustani ya Eden Bliss, Nairobi ulimwengu ukiandhimisha Siku ya Wapendanao.
Harusi ya Anne na Wilson Mutura ya awali iligharimu dola moja pekee ya Kimarekani lakini sherehe ya sasa imegharimu takriban Sh3.5 milioni (Dola 35,000).
Pesa hizo zimegharimiwa na makundi mbalimbali yanayohusika katika uandaaji wa sherehe, ambayo yaliungana kwa pamoja na kuchanga pesa kuandalia Anne na Wilson sherehe ya kukata na shoka.
Wawili hao, wanaoishi eneo la Kasarani, Nairobi, walisifiwa kwa kuonyesha thamani halisi ya mapenzi badala ya kuongozwa na pesa.
Kando na kuandaliwa harusi hiyo, wametunukiwa shamba la kilimo cha kisasa, fungate kwenye hoteli ya kifahari na baada ya sherehe ya leo wanatarajiwa kwenda kwa fungate nyingine mjini Dubai.
yenyewe walioyotumia Anne na Wilson katika harusi yao waliitumia kununua pete mbili.
yenyewe walioyotumia Anne na Wilson katika harusi yao waliitumia kununua pete mbili.
Walikuwa wameahirisha harusi yao mara tatu baada ya kukosa fedha za kutosha kuandaa sherehe kubwa ya harusi.
Maombi yao kwa familia na marafiki kuwafanyia mchango, hayakutimizwa.
Baada ya muda, Bwana harusi, Wilson, hakuwa na la kufanya ila kumshawishi mpenzi wake kuhusu uwezo wake.
"Wilson aliponieleza hali yake, sikukataa. Mapenzi yetu yalizidi yote," Ann aliambia BBC.
Wilson Muturi na mkewe Ann walitumia dola moja pekee wakati wa harusi yao |
"Mapenzi yetu yalidumu kwa muda na ili kujistiri kutoka maovu baada ya kupata baraka ya wazazi, tuliamua kufanya mambo yetu rasmi," anasema Wilson Siku yenyewe ilipofika, bwana Harusi, Wilson aliwashangaza waumini baada ya kukimbia nje sherehe ikiendelea.
"Alitoka ghafla kununua pete ya harusi nilipokuwa naendelea na shughuli ya kuwafunganisha," alisema askofu Jasper Owach, ambaye aliongoza hafla hiyo.
KWA HISANI YA BBC SWAHILI.
KWA HISANI YA BBC SWAHILI.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.