ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Wednesday, February 15, 2017

MAELLFU YA WANANNCHI WAANDAMANA NA MEXICO DHIDI YS TRUMP

MAELFU ya wananchi wa Mexico wamefanya maandamano makubwa katika mji mkuu wa nchi hiyo Mexico City wakitaka kuheshimiwa nchi yao na MAELFUwahajiri wa nchi hiyo. Maandamano hayo yamefanyika kufuatia matamshi ya chuki na uhasama ya Rais Donald Trump wa Marekani na serikali yake dhidi ya wahajiri na Wamexico.

Ripoti zinasema kuwa wafanya maandamano hao ambao jana walikusanyika kwa wingi katika mji mkuu wa Mexico huku wakiwa wamebeba bendera za nchi hiyo, wametangaza kupinga mipango ya Rais Donald Trump wa Marekani ya kutaka kujenga ukuta wa mpakani na kuendelea kuwafukuza wahajiri wa Mexico huko Marekani.


Maandamano ya wananchi wa Mexico dhidi ya Rais wa Marekani.

Jumapili iliyopita pia maaandamano mengine kama hayo yalishuhudiwa katika miji mbalimbali ya Mexico katika kupinga siasa za Marekani dhidi ya nchi hiyo. Wafanya maandamano hao walisema kuwa wao wakiwa ni raia wa Mexico wanapasa kuitolea mwito serikali itekeleze majukumu yake na kuwalinda raia na mamlaka ya kitaifa mbele ya mashambulizi ya serikali ya Marekani.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.