ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Tuesday, February 28, 2017

AIRTEL WASHIRIKIANA NA UCSAF KUFIKISHA MAWASILIANO VIJIJI 49 DODOMA.

 Mkuu wa Wilaya ya Mpwapwa Jabir Shekimweri akiongea wakati wa akizugumza na Wakazi wa kijiji cha Mbori,Kata ya Matomondo Wilayani Mpwapwa wakati wa uzInduzi wa Mnara wa Matomondo. Aidha Airtel pamoja na USCAF ilizindua minara minne wilayani hapo na kuwawezesha wakazi katika vijjiji 49 kupata huduma za mawasiliano ya uhakika
Meneja wa Kampuni ya Simu ya Airtel,Mkoa wa Dodoma Paschal Bikomagu akiongea wakati wa akizugumza na Wakazi wa kijiji cha Mbori,Kata ya Matomondo Wilayani Mpwapwa wakati wa uzInduzi wa Mnara wa Matomondo. Aidha Airtel pamoja na USCAF ilizindua minara minne wilayani hapo na kuwawezesha wakazi katika vijjiji 49 kupata huduma za mawasiliano ya uhakika
Mkuu wa Wilaya ya Mpwapwa,Jabir Shekimweri akisalimiana na mchezaji wa timu ya Manchester United ya Mbori Wilayani Mpwapwa,Juma Athmani  katika mchezo wa fainali uliochezwa juzi katika uwanja wa Ikulu kata ya Matomondo Wilayani Mpwapwa. mchezo huo ulikuwa madhumuni kwa ajili ya uzinduzi wa mnara wa simu wa Matomondo uliojengwa na Kampuni ya simu ya mkononi ya Airtel kwa kushirikiana na USCAF ili kufikisha huduma mawasiliano kwa wananchi waishio maeneo ya pembezoni mwa nchi. Manchester ilishinda kwa mabao 4-3 dhidi ya  Liverpool
Mkuu wa Wilaya ya Mpwapwa Jabir Shekimweri akisalimiana na wachezaji wa  timu ya Liverpoll ya Mbori Wilayani Mpwapwa katika mchezo wa fainali uliochezwa juzi katika uwanja wa Ikulu kata ya Matomondo Wilayani Mpwapwa.  mchezo huo ulikuwa na madhumuni kwa ajili ya uzinduzi wa Mnara wa simu wa Matomondo,uliojengwa Kampuni ya simu ya mkononi ya Airtel kwa kushirikiana na USCAF ili kufikisha huduma mawasiliano kwa wananchi waishio maeneo ya pembezoni mwa nchi. Manchester ilishinda kwa mabao 4-3 dhidi ya  Liverpool


Airtel washirikiana na UCSAF  kufikisha mawalisiano vijiji 49 Dodoma

·         Airtel na UCSAF wazindua minara minne ya mawasiliano mkoani Dodoma
·         Huduma za kifedha kupitia simu za mkononi kuboresha shughuli za kijamii na biashara kwa wakazi wa maeneo hayo
Dodoma, 24 Februari 2017,  Kampuni ya simu za mkononi ya Airtel katika mpango wake wa kufikisha huduma za mawasiliano kwenye maeneo ya pembezoni imeshirikiana na Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote (UCSAF) kwa kujenga na kukamilisha miundombinu ya mawasiliano katika kata 10 zilizoko katika maeneo ya vijijini ili kutoa huduma bora ya mawasiliano.

Katika kufanikisha mkakati huo , Airtel na UCSAF leo imefanya uzinduzi wa kwanza wa minara minne iliyoko katika kata za Matomondo, Mbuga and Ipera wilaya ya Mpwapwa mkoani Dodoma ambapo uzinduzi huo utawawezesha wakazi zaidi ya  38,000 katika vijiji 49 kuunganishwa na huduma za mawasiliano toka Airtel na kufurahia huduma na bidhaa mbalimbali ikiwemo huduma za intaneti, kupiga simu pamoja na huduma ya Airtel money ili kutatua changamoto zao

Akiongea wakati wa uzinduzi wa huduma za mawasiliano katika kata ya Matomondo Dodoma,  Meneja wa mauzo wa Airtel Dodoma, Bwn Pascal Bikomagu alisema” Airtel imejipanga katika kuboresha na kupanua upatikanaji wa huduma za mawasilino  ili kuchochea kukua kwa shughuli za kijamii na kiuchumi katika maeneo yaliyo na changamoto hususani vijijini

“Kufatia uzinduzi huu leo tunawashauri wakazi wa kata ya Matomondo na vijiji vya jirani kutumia huduma za Airtel Money katika kufanya miamala ya kifedha. Huduma hii ya Airtel Money itawawezesha kutuma na kupokea pesa, kulipia ankra mbalimbali kwa urahisi na gharama nafuu, na pia kutumiaka kama mfumo rasmi wa huduma za  kifedha kwani upatikanaji wa huduma zingine za kibenki katika maeneo hayo bado ni changamoto.” Aliongeza Bikomagu

Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Mpwapwa, Mh. Jabir Shekimweli Alisema “ mawasiliano ya simu ni nyenzo muhimu katika kukuza uchumi wa jamii na nchi kwa ujumla, nachukua fursa hii kuwahimiza wakazi wa kata za Ipera,Matomondo na Mbuga kutumia mawasiliano hayo katika kuboresha shughuli zao za kilimo na biashara ili kuinua kipato.

Naye Mkuu wa Huduma za Ununuzi na Ugavi UCSAF, John Munkondya alisema  “Tunawapongeza Airtel kwakumaliza ujenzi wa minara hii yakutoa mawasiliano bora, leo hii tumeanza kuzindua huduma za mawasilino katika mkoa wa Dodoma. ni matumaini yetu tutaendelea kushirikiana na kuboresha huduma hizi za mawasiliano ili kuwafika watanzania wengi zaidi.

Airtel ilisaini makubaliano na Serikali kupitia Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote UCSAF kwa lengo la kufikisha mawasilino katika maeneo ya pembezoni mwa nchi. Kupitia mpango huu kata 28 nchini zimeweza kufikiwa na hivyo kuongeza idadi ya minara ya mawasiliano ya Airtel kufikia 2,210 ndani ya miji zaidi 128 na hivyo kuwafikishia huduma za mawasiliano wakazi zaidi ya  asilimia 85 nchin.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.