NA K-VIS BLOG/Khalfan Said
SHIRIKA la Umeme Tanzania, (TANESCO), limeeleza chanzo cha
kukatika umeme leo Januari 25, 2017), ni kulipuka kwa kikata umeme,(Circuit
breaker), baada ya kifaa kijulikanacho kama female connector ya umeme wa 132kv kutoka
kituo cha kupoza umeme cha Ubungo jijini Dar es Salaam kwenda Chalinze mkoani Pwani kupata hitilafu.
Kwa mujibu wa Kaimu Meneja Mwandamizi udhibiti mifumo ya umeme TANESCO
makao makuu, Mhandisi Abubakar Issa,(pichani juu), alisema hitilafu hiyo iliyotokea majira ya
saa 12;32 asubuhi, leo Januari 25, 2017 ilileta athari kwenye mfumo mzima wa gridi ya taifa na
kufanya wateja wa TANESCO walio kwenye mikoa inayotumia gridi ya taifa kukosa
umeme kwa takriban masaa mawili.
"Napenda kuwahakikishia wateja wetu kuwa gridi ya taifa iko salama, hakuna tatizo lolote isipokuwa ilizima baada ya kikata umeme hicho kulipuka, lakini sasa mambo yamewekwa sawa na umeme unazidi kurejea katika hali yake ya kawaida kote nchini" alisema Mhandisi Issa, wakati waandishi wa habari walipopelekwa kujionea wenyewe hitilafu hiyo majira ya mchana leo.
Hata hivyo alisema kifaa kilichoharibika kinasafirishwa kutoka
mkoani Tanga, na mara kitakapowasili kitafungwa mahala kilipoharibika kile cha awali.
|
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.