ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Wednesday, January 25, 2017

WANAFUNZI 900 KUJENGEWA MADARASA

NA ANNASTAZIA MAGINGA,Mwanza

HALMASHAURI ya jiji la Mwanza inatarajia kujenga madarasa manne yatakayo gharimu Sh. 80 milioni katika shule ya msingi Buhongwa baada ya kuwa na ongezeko la wanafunzi.

Imeelezwa kuwa walioandikishwa kuanza darasa la kwanza  na walioko la  pili  wamefikia 900 idadi ambayo ni ya shule nzima lakini kwa shule hiyo hali imekuwa tofauti kutokana na muamko wa wazazi kuandikisha watoto kwa wingi.

Akizungumza na waandishi wa habari Mkurugenzi wa jiji hilo Kiomoni Kibamba amesema ujenzi huo utaanza kwa haraka kutokana na mahitaji yaliyopo ingawa upungufu wa madarasa kwa shule zote za msingi ni 1261.

“Watoto walioandikishwa darasa la kwanza mwaka huu wako 400 ,la pili 500 kwa hiyo jumla ni 900 idadi ambayo pengine ni ya shule nzima kwa hiyo inatulazimu kujenga madarasa kwa haraka ili watoto wasome”amesema Kibamba.

Amesema kwa sasa wanafunzi hao wanasoma kwa awamu ili kukidhi mahitaji na kwamba walikuwa wamejipangia kujenga madarasa 50 mwaka huu ambayo yangegharimu Sh. Bilioni 1 kutokana na mapato ya ndani lakini fedha hizo zilibadilishwa matumizi na kutengeneza madawati 9,000 huku hadi sasa yamekwisha tengenezeka 12,000 na upungufu yakiwa 13,500.
Mwisho.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.