Countinho atapokea kitita cha pauni 150,00 kwa wiki, na kumfanya kuwa mchezaji anayelipwa kiwango cha juu zaidi katika klabu hiyo.
Mchezaji huyo wa kimataifa kutoka Brazil mwenye miaka 24, alijiunga na majogoo hao wa Anfield kutoka Inter Milan kwa pauni milioni 8.5 mwezi Januari mwaka 2013.
Mkataba huu mpya utamfanya mshambuliaji huyo kusalia na klabu hiyo hadi mwaka wa 2022.
Coutinho amefunga mabao 34 katika mechi 163 alizoshiriki na Liverpool.
''Ni klabu ambayo naishukuru sana, ndiyo inayodhihirisha furaha yangu hapa,'' aliiambia mtandao wa klabu hiyo.
Hakuna kifungu chochote kuhusu kuondoka kwake kwenye mkataba wa Countinho, ambao utaanza kutekelezwa rasmi mwezi Julai.
Countinho alisemekana alikuwa na matamanio ya kuihamia klabu ya Uhispania ya Barcelona.
Countinho alisemekana alikuwa na matamanio ya kuihamia klabu ya Uhispania ya Barcelona.
''Nimesaini mkataba huu mpya kusalia na klabu hii kwa miaka mingine kadhaa, kwa sababu ni heshima kubwa kwangu.
''Nafasi hii imenipatia furaha , kwa sababu nilikaribishwa kwa mikono miwili na kila mmoja katika klabu hii na pia mashabiki tangu siku yangu ya kwanza.''
Coutinho alinunuliwa na meneja wa zamani Brendan Rodgers, wakati Southampton pia walipotaka kumsajili wakati huo.
Mshambuliaji huyo alijiwasilisha kama kiungo muhimu wa Reds kwa miaka minne huko Anfied.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.