- Fedha hizo zilinaswa mnamo tarehe 4 January 2017.
Ofisi za majaji huko kaskazini mashariki mwa marekani siku ya Jumatatu waliandika ujumbe kupitia mtandao wa twitter zikionyesha maburungutu ya noti yakiwa katika box.
Pesa hizo zilikamatwa january 4,na Cleber Rocha(mtuhumiwa) alidaiwa kwa kosa la kuficha pesa kesi ambayo ilisikilizwa mahakamani huko Massachusetts.
Lakini kwa mujibu watu wa usalama jamaa huyo alitumwa na binamu yake ambaye pia ni mwenye asili ya brazili na anafanya shughuli za kusafirisha mabillion ya pesa kwanjia za kinyemela.
Hivyo Carlos ambaye ni binamu wa bwana Rocha alisafiri kutoka Brazil nakupitia Canada ili kukwepa kukamatwa ,wakati mwenzake bwana James Merril akiwa amejisalimisha na kusubiri kusomewa kesi.
Hivyo inasemekana bwana Carlos alikuwa na pesa nyingi zaidi alizotaka kuzisafirisha bado zimefichwa maeneo ya Boston huko marekani.
Lakini bwana Rocha anaweza akakutana na kifungo kisichopungua miaka 20,kama atapatikana na hatia kuhusu sakata hilo.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.