ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Monday, January 16, 2017

LOWASSA AKAMATWA GEITA.

Waziri Mkuu mstaafu na aliyekuwa mgombea urais kwa CHADEMA Mh. Edward Lowassa na mbunge wa Geita (M) Viti maalum Upendo Peneza wamekamatwa  na jeshi la Polisi Geita mjini.
Taarifa zinaarifu kuwa  Lowassa amefika Geita leo akitokea Kagera  ambapo alipofika stendi ya zamani Geita wananchi walimsimamisha. Aliposhuka kwenye gari kuwasalimu wanageita, polisi wakamkamata na kumpeleka kituo cha Polisi Geita.

Lowassa alikuwa anaenda kwenye kampeni za uchaguzi Kata ya Nkome

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.