ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Monday, January 2, 2017

MASKINI....MADAWA YA KULEVYA YAMMALIZA MSHIRIKI WA BIG BROTHER AFRIKA 'NANDO'....ACHAKAA VIBAYA .AWA OMBAOMBA CLUB

Mshiriki wa shindano la Big Brother Africa ‘The Chase’, Ammy Nando khali yake yazidi kuwa mbaya yasemekana ni kutokana na matumizi ya dawa za kulevya. 

Nando ambaye hupendelea kutembelea club za samaki samaki na eaters masaki nyakati za usiku huonekena akiwa anaranda randa maeneo hayo huku akiwa na bia mkononi ajabu zaidi hata muonekano wake umebadilika kutokana na kuwa rafu (mchafu) tofauti na alivyo kuwa amezoeleka nyakati za nyuma kwa usafi.
Hata hivyo mwaka juzi alisha wahi hojiwa na vyombo vya habari na  kusema 'Nimeacha Kutumia Madawa ya Kulevya, Ila Bagi ni Moja au Mbili kwa Siku'

Jamani ni matumaini yetu sote kumsaidia huyu kijana kwani khali yake ya sasa si nzuri hata kidogo.
Enzi zake katika ushiriki wa Big Brother Africa, Nando alikuwa makini na mtu wa kijutambua naye alipeperusha vyema bendera ya Tanzania kwenye ushiriki wake ingawa hakushinda kwenye kinyang'anyiro.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.