ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Monday, January 2, 2017

"YUMKINI MAREKANI NA RUSSIA ZIKAINGIA VITANI NDANI YA SIKU 20 ZIJAZO"

Marekani ipo katika ncha ya kungia kwenye vita na Russia katika kipindi cha siku 20 zijazo.
Hayo yamesemwa na mwandishi wa habari na mchambuzi wa kisiasa mkazi wa mji wa New York ambaye ameongeza kuwa, kutokana na kushtadi uadui wa Marekani dhidi ya Russia, nchi mbili hizi huenda zikaingia vitani kabla ya Januari 20, wakati ambapo Rais Barack Obama anajiandaa kuondoka Ikulu ya White House.
Don DeBar, mtangazaji wa radio mjini New York na mchanganuzi wa masuala ya siasa za kimataifa amefafanua katika mahojiano yake na kanali ya televisheni ya Press TV ya Iran kuwa: "Kuna uwezekano mkubwa Marekani ikaingia katika vita na Russia kabla ya Trump kuchukua rasmi hatamu za uongozi."
Wanajeshi wa Marekani katika eneo la Balkan
Ameongeza kuwa, vikosi vya jeshi la Marekani katika muda wa mwaka mmoja na nusu, vimetumwa katika Peninsula ya Korea na eneo la Balkan katika mpaka wa Russia na tangu wakati huo vimekuwa vikifanya luteka za kijeshi na nchi za eneo hilo.
Mwanahabari huyo wa Marekani amesema msuguano wa kidiplomasia wa hivi karibuni kati ya Washington na Russia huenda ukawa chachu za kuzifanya nchi mbili hizo wanachama wa kudumu wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kuingia vitani kabla ya Januari 20, huku akitoa wito wa kuchukuliwa hatua za dharura kukomesha hatari ya nchi hizo kuhujumiana.
Rais Vladimiri Putin wa Russia (Kushoto) na Barack Obama wa Marekani

Siku chache zilizopita, serikali ya Rais Barack Obama iliwatimua nchini Marekani wanadiploamasia 35 wa Russia sanjari na kuwawekea vikwazo maafisa sita pamoja na mashirika matano ya Russia kama jibu kwa madai kuwa Moscow ilidukua mfumo wa upigaji kuwa Marekani na kuchakachua matokeo ya uchaguzi wa hivi karibu wa rais kwa maslahi ya Donald Trump.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.