Le Monde limeandika kuwa, licha ya mjada mkubwa uliohusu kuchaguziliwa kwa Donald Trump kuwa Rais mpya wa Marekani, Vladimir Putin ndiye mtu mashuhuri zaidi katika mwaka huu wa 2016.
Le Monde limeongeza kuwa, katika kipindi chote cha miaka 16 ya uongozi wake, Putin ameweza kuwa na nafasi muhimu nchini Russia na ulimwenguni.
|
Vladimir Putin |
Gazeti hilo limeandika kuwa, licha ya mivutano iliyopo baina ya Rais wa Rusia na Umoja wa Ulaya lakini Putin ameweza kuimarisha uhusiano wa kistratijia na vyama na wanasiasa wakubwa wenye mielekeo kama yake barani Ulaya. Le Monde limeongeza katika tahariri yake kwamba, ushawishi wa Rusia katika duru za kiutamaduni na kisiasa barani Ulaya umeongeza kwa kiwango kikubwa katika mwaka huu wa 2016.
|
Barack Obama na Vladimir Pitin |
Uhusiano wa Russia na Umoja wa Ulaya na Marekani ulivurugika baada ya machafuko ya ndani nchini Ukraine na kuwa mbaya zaidi baada ya Russia kuliunganisha eneo la Crimea na ardhi yake.
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.