ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Monday, December 12, 2016

TRUMP AKEJELI MADAI KUWA URUSI ILIVURUGA UCHAGUZI.

Trump awakosoa majasusi wa Marekani
Trump awakosoa majasusi wa Marekani.
CHANZO:- BBC SWAHILI.
Donald Trump ametoa shutuma mpya kupinga madai ya ujasusi nchini Marekania kuwa wadukuzi nchini Urusi waliingilia uchaguzi wa Marekani.
Rais huyo mteule wa Marekani pia aliuliza kuhusu ni kwa nini madai hayo ya udukuzi hayakutolewa kwa umma kabla ya kufanyika kwa uchaguzi.
"Kabla wadukuzi hawajakamatwa kwenye kitendo, ni vigumu sana kubaini ni nani alikuwa akidukua. Mbona hili halikusemwa kabla ya uchaguzi?" Trump aliandika kwenye ukurasa wake wa Twitter leo Jumatatu.
Vinyago vya Urusi kwenye duka mjini Moscow
Vinyago vya waheshimiwa kwenye duka mjini Moscow.

Siku ya Ijumaa maafisa wa CIA walivyambia vyombo vya habari nchini Marekani kuwa, wadukuzi wa Urusi walijaribu kuvuruga uchaguzi na kumpendelea Trump.
Timu ya ilijibu madai hayo na kusema: "Hawa ni sawa na wale watu waliosema kuwa Saddam Hussein alikuwa na silaha za maangamizi."
Trump yuko nyuma ya Trump katika wingi wa kura kwa karibu kura milioni 2.8 licha ya yeye kushinda kwa kura nyingi zaidi za wajumbe katika historia ya Marekani.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.