LIVE KUTOKA KILOLELI.
| Ni changamoto kubwa sana kwa wadau hawa kuanza safari mpya ya maisha kibiashara. |
| Akinamama wenye watoto wao mgongoni na vijana wadogo wameonekana eneo hili wakisota kuchimba mashimo ya kusimika nguzo kwaajili ya kujenga upya vibanda vya biashara eneo hili la Kiloleli. |
| Ulinzi mkali umeimarishwa hapa, wakati huo huo manung'uniko ya baadhi ya wafanyabiashara yakijikita kukosa maeneo ya kufanyia biashara. |
| Hakuna Fundi, Pichani, "Pale akinamama na akinadada zetu wanapogeuka kuwa mafundi ujenzi" |
| Kazi mpya kama inachosha hivi. |
| Sawa wafanyabiashara hawa wameletwa hapa Kiloleli, lakini pia kumbuka kulikuwa na watu hapa, Jeh waliokuwa hapa wamepewa kipaumbele au nao waliandikishwa upya? |
| Vijana kizazi kipya na harakati za kusaka maisha mapya... kwa mbaaaaaali ulinzi mkali. |
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment