NA VICTOR MASANGU, RUFIJI
IMEELEZWA kuwepo kwa sakata la kutokea kwa migogoro ya ardhi kila kukicha katika Wilaya ya Rufiji Mkoa wa Pwani kunachangiwa kwa kiasi kikubwa na baadhi ya watendaji wa vijiji kuendekeza masuala ya rushwa ,ufisadi na kuuza maneo kiholela hali ambayo inasababisha kuchochea vurugu na mapigano ya mara kwa mara kati ya jamii ya wakulima na wafugaji .
Hayo yamebainishwa na Mbunge wa Jimbo la Rufiji Mohamed Mchengerwa wakati wa ziara yake ya kikazi kwa ajili ya kuweza kukagua shughuli mbali mbali za kimaendeleo pamoja na kuona changamoto zinazowakabili wananachi wake ili kuweza kuona namna ya kuzitafutia ufumbuzi.
Mchengerwa alisema kwamba katika Jimbo lake la Rufiji kumekuwepo na baadhi ya wenyeviti wa vijiji na watendaji kuwa na tamaa kwa kuamua kuuza hekari moja ya ardhi kwa kiasi cha shilingi elfu tisa hali ambayo amedai hawezi kuwavumilia na atakikisha anashirikiana na viongozi wa serikali kuvunja mikataba yote kwa wawekezaji waliojipatia maeneo kinyume cha sheria.
“Jamani wananchi wangu kwa hili suala mimi siwezi kukubaliana nalo hata kidogo yani baadhi ya watendaji wa vijiji wanafanya mambo kinyume cha sheria na taratibu kabisa, wanauza ardhi kwa bei ya shilingi elfu tisa, hapa hili nitalivalia njuga na wawezezaji wote walionunua maeneo inabidi tukae nao tena chini kuwekeana mikataba hii sio sahihi hata kidogo,”alisema Mchengerwa.
Aidha Mchengerwa katika hatua nyingine alisema kutokana na kuwepo na hali ya sintofahamu kwa wananchi wa kata nzima ya Chumbi kuhusiana na suala zima la baadhi ya watendaji wa kijiji hicho kutuhumiwa kuhusika kujihusisha na uuzaji wa maeneo na kufanya ubadhilifu wa fedha amewataka kutomkaribisha mwekezaji wa yoyote mpaka Mkuu wa Mkoa wa Pwani Injia Evarist Ndikilo atapokwenda kusikiliza kilo chao na kulitatua sakata hilo la ardhi.
Pia Mchengerwa alisema kuwa maeneo mengi yameuzwa bila ya kuzingatia sheria na taratibu, hivyo katika eneo la kijiji cha Chumbi anatambua kuna migogoro mingi ya ardhi hiyo katika kulitataua suala hilo atahakikisha anashirikiana na viongozi wa ngazi ya Mkoa kwa lengo la kuweza kurudisha ardhi ambayo imechukuliwa.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa kijiji cha Chumbi Salumu Mtimbuko ambaye pia ni Diwani wa kata ya Chumbi baada ya kutuhumiwa kuhusika katika uuzaji wa ardhi kiholela na ubadhilifu wa fedha na wananchi alisema kwamba kuna baadhi ya wawekezaji wamenunua zaidi ya hekari 2900 wakati yeye bado ajaingia maadarakani.
WANANCHI wa kijiji cha Chumbi A,B,na C kata ya Chumbi Wilayani Rufiji Mkoa wa Pwani kwa sasa wanakabiiwa na sakata la kuwepo kwa migogoro mikubwa ya ardhi inayosababishwa na baadhi ya viongozi wa kijiji kujiuzia maeneo kiholela bila ya kuzingatai sheria na taratibu zilizowekwa hali inayopelekea kuwepo kwa uvunjifu wa amani.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.